Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Absolom Kibanda akimkabidhi maoni ya
Jukwaa hilo kuhusu katiba Mpya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo
(Alhamisi, Jan 10, 2013) .
Mwanachama wa Jukwaa la Wahariri (TEF)
Bw. Deodatus Balile akiwasilisha maoni ya Jukwaa hilo kuhusu Katiba
Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam leo (Alhamisi, Jan 10, 2013). Wengine ni Bw. Ruge Mutahaba
(kushoto) kutoka Clouds Media Group na Bw. Yasin Sadik kutoka gazeti la
Hoja.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari
Tanzania (MCT) Bw. Kajubi Mukajanga akiwasilisha maoni ya Baraza hilo
kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume
jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Jan 10, 2013). Kulia ni Bi. Pili
Mtambalike kutoka MCT.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa
Vyombo vya Habari (MOAT) Bw. Reginald Mengi akitoa maoni ya chama hicho
kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo
(Alhamisi, Jan 10, 2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo Prof. Palamagamba Kabudi.Source Mjengwa.
Comments