Bunge la Venezuela litaanza kikao huku wasiwasi ukizidi ikiwa Rais Hugo Chavez ataweza kuanza muhula wake wa pili wa uongozi au la.
Bwana Chavez anauguzwa Cuba baada ya kufanyiwa
upasuaji kutoa saratani, na inafikiriwa huenda akawa mgonjwa sana na
hataweza kuhudhuria sherehe ya kuapishwa juma lijalo.
Hata hivo makamo wa rais, Nicolas Maduro,
alisema Bwana Chavez anaweza kuapishwa baadae mbele ya mahakama makuu,
na alikataa wito wa upinzani kwamba kufanywe uchaguzi mwengine.
Mwandishi wa BBC, Sarah Grainger, akiwa mjini
Caracas, anasema ufunguzi wa kawaida wa bunge la taifa umekuwa muhimu
safari hii kwa sababu ya Bwana Chavez kukosekana.Source BBC.
Comments