Na Majid Ahmed, Mogadishu
Viongozi wa al-Shabaab wamefichua hali mbaya kifedha ya kikundi chao
baada ya kufanya mfululizo wa maombi katika miezi kadhaa iliyopita kwa
makabila ya Somalia na wafanya biashara ili watoe msaada wa kifedha kwa
shughuli zao za kigaidi, kwa mujibu wa wachambuzi na waangalizi wa
masuala ya kisiasa wa Somalia.
Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia na
mwanachama wa Brigedi ya Ras Kamboni inayoiunga mkono serikali
wakiangalia juu ya gati ilioko katika mji wa bandari wa Kismayu, ngome
imara ya zamani ya al-Shabaab. [Na AU-UN IST/AFP]
Katika ujumbe wa sauti uliotolewa mwezi wa Disemba na al-Kataib Media
Foundation, tawi la habari la al-Shabaab, kiongozi wa al-Shabaab Ahmed
Abdi Godane, anayejulikana pia kama Mukhtar Abu al-Zubair, alikubali
kadamnasi kuwa wapiganaji wa al-Shabaab walikuwa wameshindwa katika
mfululizo wa vita dhidi ya vikosi vya Somalia na washirika wake. Katika
ujumbe huo, aliwataka watu wa Somalia kusimama imara na kukisaidia
kikundi chao kifedha.
"Ninapenda kuwaambia Waislamu wa Somalia kusimama imara kwa ndugu zenu
waaminifu wa mujahidina na muwape fedha kwa vile wanapigana kuulinda
Uislamu," alisema.
Ali Mohamed Hassan, mwakilishi wa zamani wa al-Shabaab huko mkoa wa
Banadir, aliwataka wakaazi na wafanyabiashara wa Mogadishu hapo tarehe
25 Disemba watoe msaada wa kifedha kwa al-Shabaab ili iweze kugharamia
operesheni zao za kijeshi. "Tunawataka wafanyabiashara wawasaidie
mujahidina na watoe fedha zao kwa jina la Mwenyezi Mungu," alisema.
Hata katika ya miezi ya kabla ya Juni, kabla ya kikundi kuipoteza
kimkakati Kismayu, Godane aliyataka makabila ya Somalia kuunga mkono
kikundi cha wanamgambo dhidi ya serikali ya Somalia.
Chini ya wiki moja baadaye,Yusuf Sheikh Isse, kiongozi wa al-Shabaab katika mkoa wa Shabelle ya Kati, aliyatolea wito makabila na wafanyabiashara kufanya michango ya kifedha kwa ajili ya operesheni za kikundi.
Chini ya wiki moja baadaye,Yusuf Sheikh Isse, kiongozi wa al-Shabaab katika mkoa wa Shabelle ya Kati, aliyatolea wito makabila na wafanyabiashara kufanya michango ya kifedha kwa ajili ya operesheni za kikundi.
Comments