WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. mwananchi
Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli
hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.
“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga
rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe.
, ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na subira
katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna
gesi asilia.
Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi kutambua
kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni mali ya Watanzania wote na
siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.
Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi,
kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano yasiyokuwa na
msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza rasilimali za wananchi
bila faida.
Comments