Na Rajab Ramah, Nairobi
Unganishwaji wa intaneti ulioboreshwa nchini Kenya unaongeza ukuaji wa
uchumi, kupatikana kwa kazi na kuongeza upataji wa elimu, maofisa
wahusika wa tasnia hiyo wamesema.
Mem Maina akionyesha matumizi ya simu mpya
wakati wa maonyesho ya teknolojia ya Afrika ya DEMO kwenye Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta jijini Nairobi tarehe 25 Oktoba.
Utafiti wa hivi karibuni ulionyesha kwamba simu za mkononi zinaweza
kusaidia kuondoa pengo linalotenganisha la dijitali na kutoa ufikivu wa
intaneti kwa Wakenya wengi zaidi. [Simon Maina/AFP]
Huduma za mtandao zinazopatikana kwenye kompyuta na simu za mkononi
zimepunguza gharama za muamala katika sekta mbalimbali na kusaidia
kufanya maisha ya raia kuwa rahisi, kwa mujibu wa mwenyekiti wa Chama
cha Walaji cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Alex Gakuru.
"Wananchi wanaweza kupakua na kujaza nyaraka muhimu kama vile ripoti ya
polisi kwa kubofya kipanya," aliiambia Sabahi. "Wanaweza kulipa bili kwa
kutumia simu zao za mkononi na wanaweza kuomba kazi kupitia mtandao.
Hii inamaanisha kwamba inapunguza kusafiri na matumizi."
Kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Mawasiliano ya Kenya ya 2011-2012
iliyotolewa Oktoba, matumizi ya intaneti kupitia kompyuta za kawaida
yamekua kwa watumiaji milioni kwa silimia 19.2 hadi 7.7, wakati matumizi
ya inteneti kwa njia ya simu za mkononi yamekua kwa watumiaji milioni
kwa asilimia 1.7 hadi 29.7.
Ingawaje gharama kubwa za ufikiaji zimeendelea kuwepo, Gakuru alisema,
kuogezeka kwa uingiaji kwenye intaneti umeboresha biashara, mawasiliano
na mandhari ya elimu nchini Kenya.
Uunganishwaji mzuri umetafsiriwa kwenye gharama ndogo za matangazo kwa
ajili ya biashara, kwani sasa wanaweza kufikia watu wengi kupitia
mtandao. Kuwasiliana na wateja kupitia mtandao, ambao wanatoa mwitikio
kwa wamiliki wa biashara, husaidia malengo ya kampuni na kukidhi vizuri
matakwa ya wateja, Gakuru alisema.
Comments