Na Rajab Ramah, Nairobi
Osewe Ramogi anaelezea polepole mazingira ya wazi aliyoyashuhudia wakati
wa kilele cha vurugu za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007, wakati
vijana walizivamia makazi duni jijini na kuchoma moto majumba na kupora,
na kuwafadhaisha wananchi waliowadhania kuwa hawakuwaunga mkono
wagombea wao.
Mkenya na watoto wake wakitoroka makazi
duni ya Mathare mjini Nairobi mwezi Januari 2008 ili kuepuka vurugu
zilizolipuka baada ya uchaguzi. [Na Tony Karumba/AFP]
"Nimejaribu kuzifuta picha kutoka kumbukumbu zangu lakini zinakuwa
zikijirejea akilini kila mara," alisema Ramogi, mwenye umri wa miaka 30
anayeishi katika makazi duni ya Kibera. "Waliwafukuza wale waliodhani
kuwa kikabila ni tofauti na kamwe hawakumuunga mkono mgombea maalumu.
Tuliachwa na maisha yaliyozorota na vifo baada ya vurugu hizo."
Ramogi, mwanachama wa Chini ya Anga Moja-Kenya, kikundi cha vijana wa
makazi duni ya Kibera ambacho kinashughulikia mazingira ya eneo lao na
matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa, alisema kuwa kwa miaka mingi
wanasiasa wamekuwa wakijishughulisha na kampeni kwa umma za kuwachochea
watu katika makazi duni kufanya fujo kwa faida zao wenyewe za kisiasa.
"Ukabila una umuhimu mkubwa katika siasa za Kenya tangu uhuru mwaka
1963, na inaelekea kuwa ukabila ndio msingi muhimu wa maamuzi ya
kisiasa," alisema.
Lakini huku Kenya ikijitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa tarehe 4 Machi,
Ramogi alisema kuwa vijana kutoka makazi kadhaa duni ya Nairobi
wanakutana ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayetumiwa tena kama rehani
wa kisiasa.
Hapo mwezi Januari 2012, Ramogi aliunda jukwaa la Mazungumzo na
Maridhiano ya Amani Kwa Vijana wa Makabila Mbalimbali pamoja na idadi
kadhaa ya vikundi vyengine vya vijana vinavyoshugulikia migawanyiko ya
kikabila ambayo bado ilikuwa inaendelea katika makazi duni ya Kibera
miaka kadhaa baada ya uchaguzi wa 2007.
Comments