Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Abdulrahman Kinana |
SAKATA la gesi sasa limeingia hatua mpya, baada ya watendaji wakuu wa
CCM; Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye kuitaka Serikali ikae na wana-Mtwara ili kuona namna ya
kumaliza mgogoro huo kwa amani.
Kinana na Nape walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana. Wakati
Kinana alisema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara
mkoani Kigoma, Nape alifanya hivyo kupitia mtandaowa Twitter na baadaye
kuthibitisha kauli hiyo alipoulizwa na mwandishi wetu.
Wakati watendaji hao wa CCM wakitoa matamko hayo, Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda jana alifanya vikao mfululizo mkoani Mtwara akisaka suluhu ya
mgogoro huo.
Kinana na Nape
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Ofisi za CCM
Wilaya ya Uvinza, Kigoma, Kinana aliitaka Serikali isikilize hoja za
wakazi wa Mtwara na kuzitafutia usumbufu sahihi.
Mbali na kutoa ushauri huo, aliitaka pia Serikali kuwasaka watu
wanaochochea mgogoro huo kwa kufanya vurugu na kuharibu mali za watu na
kuwafikisha mbele ya sheria.
“Serikali ikae na wana-Mtwara na kuwasikiliza, wananchi hao wana hoja na
Serikali inapaswa kutoa majibu sahihi kwa hoja hizo. Lakini pia iwasake
na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha uvunjifu wa amani,”
alisema Kinana.
Comments