Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS yakutana kujadili mzozo unaoendelea nchini Mali
Kulia ni Mwenyekiti wa ECOWAS Alassane Quattara akiwa
na Rais wa mpito wa Mali Dioncouda Traore
Reuters/Luc Gnago
|
Na Flora Martin Mwano
Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi ECOWAS inafanya kikao cha
dharura jijini Abdijan nchini Cote d'Ivoire leo jumamosi kujadili hali
inavyoendelea nchini Mali. Kikao hicho kinafanyika chini ya Mwenyekiti
wa ECOWAS Allasane Outtara ambaye pia ni Rais wa Cote d'Ivoire.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Ufaransa Laurent Fabius ni miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria kikao hicho jijini Abdijan.
Jana ijumaa vikosi vya kijeshi vya Mali vikishirikiana na Ufaransa
ziliendeleza makabiliano na kufanikiwa kuudhibiti mji wa Konna uliokuwa
unamilikiwa na wapiganaji wa kiislamu walioshikilia eneo la kaskazini
mwa nchi hiyo toka mwaka jana.
Jeshi la Mali na Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa kwa pamoja wamethibitisha
kufanikiwa kuudhibiti mji huo uliopo umbali wa kilometa mia saba kutoka
katika mji mkuu wa nchi hiyo Bamako.
Hofu ya ukiukwaji wa haki za binadamu imezidi kutanda wakati ambapo
maelfu ya raia wanazidi kuyakimbia makazi yao wakihofia mapigano
yanayoendelea.
Via kiswahili.rfi.fr
Comments