Marais Joseph Kabila-Kulia, Paul Kagame na Yoweri Museveni-Katikati wakiwa Kampala Uganda
REUTERS/Presidential Press Unit/Handout
Na Victor Robert Wile
Rwanda haitaunga mkono mpango wa Umoja wa Mataifa kutumia Ndege maalum
za uchunguzi zisizo na marubani dhidi ya Waasi wa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo wanaondeleza vitendo vya uasi.
Nchi ya Rwanda haitaunga mkono matumizi ya ndege hizo mpaka pale
utakapotolewa ufafanuzi juu ya maswali yao kuhusu namna ambavyo zoezi
hilo litakavyotekelezwa.
Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Louise Mushikiwabo ameeleza kuwa ametoa
msimamo huo wa nchi yake huku kukiwa na maswali ya kwa nini Rwanda
haiungi mkono hatua hiyo.
Umoja wa Mataifa hivi sasa una mpango wa kuliongezea nguvu jeshi lake la
kulinda amani nchini Kongo ambako hivi sasa Waasi wa M23 wamedhibiti
eneo la jimbo la kaskazini eneo lililo mpakani mwa Kongo na Rwanda.
Muungano wa Mashirika ya kiraia katika Jimbo la Kivu ya kaskazini
unaeleza uamuzi wa Rwanda kutounga Mkono mpango wa Umoja wa Mataifa
unatokana na uoga wa Rwanda kufichuliwa kile ambacho imekuwa ikikifanya
nchini DRC.
Katika ripoti mbalimbali zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, Rwanda chini
ya Rais Paul Kagame imekuwa ikitajwa kuhusika na harakati za kuwasaidia
waasi wa M23 kupambana namajeshi ya Serikali ya Joseph Kabila huku
Uganda nayo ikigusiwa kuhusika.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr
Comments