Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2018

Dkt. Regnald Mengi kuptia IPP Touchmate Ltd amewekeza bilioni II.5 kuzalisha bidhaa mbalimbali za Kielektroniki.

Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Dkt. Regnald Mengi ametangaza ujio wa Kampuni Mpya ya IPP Touchmate Ltd ambapo amewekeza bilioni II.5 kwa ajili  ya kuzalisha bidhaa mbalimbali za Kielektroniki. Kampuni hiyo itakuwa ya kwanza Tanzania kuanza kuzalisha bidhaa za Kielektroniki ikiwemo simu za mikononi, simu janja (Smartphones), Computers, Ipads, music bluetooth speakers, headphones pamoja na earphones. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Dkt. Mengi, amesema kuwa lengo kuanzisha kampuni hiyo kuendelea kukuza uchumi wa viwanda pamoja kuzalisha ajira hasa kwa watu wenye ulemavu. Amesema kuwa kiwanda hicho kinatarajia kutoa ajira rasmi na zisizo rasmi 2,000 jambo ambalo litapunguza changamoto ya kukosefu wa ajira kwa serikali. "Kampuni hii itatoa kipaombele katika kuajiri wenye ulemavu, wenye sifa stahiki" amesema Dkt. Mengi. Meneja wa IPP Touchmate Ltd Victor Tesha, amesema kuwa kiwanda hicho kitakuwa maeneo ya Mikocheni jijini

Pharrell Williams aingia mzozo na Rais Trump

Mwanamuziki na Muandaaji wa muziki nchini Marekani, Pharrell Williams amemlima barua Rais wa Taifa hilo, Donald Trump inayomtaka asitumie tena wimbo wake wa ‘HAPPY’ kwenye shughuli zake za kisiasa. Pharrell Williams Pharrell amechukua maamuzi hayo, baada ya Rais Trump kuutumia wimbo huo Wikiendi iliyopita katika Mkutano wake wa Kisiasa mjini Pittsburgh katika eneo ambalo masaa machache yaliyopita kabla ya mkutano huo, kulitokea mauaji ya watu 11 katika Sinagogi la Wayahudi. “ Siku hiyo hiyo ndani ya eneo moja, watu 11 wameuawa halafu masaa machache unacheza wimbo wa Happy inaingia akilini? tena kwenye masuala ya kisiasa. Sisi kama wanasheria tumeafikiana na Mteja wetu kuwa Rais huyo asiutumie tena wimbo huo na akirudia kufanya hivyo tutampeleka mahakamani kwa makosa ya Copyrights na ‘trademark rights’, “ameeleza Mwanasheria wa Pharrell Williams aliyejitambulisha kwa jina la Howard King. Mwanasheria huyo amedai kuwa kitendo cha Trump kucheza wimbo huo jukwaani, ni

Mabao ya Samatta yamfungisha virago kipa

Baada ya kupokea kipigo cha mabao mawili kutoka kwa nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta kwenye mchezo uliyomalizika kwa 4 – 2 mlindalango Loris Karius sasa kurejeshwa Liverpool. Klabu ya Besiktas imenuia kumrejesha kipa huyo, Karius ambaye yupo hapo kwa mkopo wa miaka miwili akitokea Liverpool na badala yake wakimhitaji Divock Origi. Miamba hiyo ya Uturuki imeripotiwa kuwa imechoshwa na huduma yake na hivyo tayari imefanya mazungumzo na Liverpool kuona namna ya kumrejesha ili kubadilishana na Divock Origi. Karius ambaye ameonekana kutokuwa na matokeo mazuri toka kutua kwake ndani ya klabu ya Besiktas haswa matokeo mabovu ya Europa League dhidi ya KRC Genk ambapo alikubali kipigo cha mabao 4 – 1 huku mshambuliaji hatari wa Tanzania Mbwana Samatta akiweka kimyani mabao mawili atarejea Anfield mwakani mwezi Januari. Mlindalango huyo raia wa Ujerumani yupo kwenye miamba hiyo ya soka ya Uturuki kwa mkopo wa miaka miwili ambayo timu hiyo amepewa nafasi ya kumnunua

Vodacom yasherehekea‘ubora wa utoaji huduma kwa wateja’

Katika kuadhimisha miaka 18 ya utoaji huduma kwa wateja wao Vodacom Tanzania (PLC)yafanyamwezimzimawa October kuwa mwezi wa huduma kwa wateja. Vodacom, imeendeleza sherehe za wiki ya huduma kwa wateja,ambazo huadhimishwa wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, na mwaka huu kaulimbiu ikiwani ‘ Kusherehekea ubora wa utoaji huduma ’. Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni ya Vodacom Tanzania , Bi. Harriet Lwakatare, amebainisha kuwa,lengo kuu la kuendeleza maadhimisho hayo ni kuwashukuru wateja wao, watoa huduma na kuonyesha huduma mbalimbali wanazozindua kwa dhumuni la kuwasaidia wateja. “Tunafurahia kuona Vodacom inaongoza katika kubadilisha maisha ya Watanzania zaidi ya milioni 12 na kuwaunganisha popote duniani. Hudumazetu zimekuwa za kwanza nchini, zimepokelewa vizuri na kuendelea kutufanya Mtandao bora wa simu nchini.” Akiongelea mchango wa hudumazao kwa watanzania na uchumi kwaujumla, Harriet alisema kuwa“MPesa imekuwa msaada mkubwa kwa huduma zakifedha k

Maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano baina ya China na Tanzania yaliyofanyika Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania imeipongeza serikali ya watu wa china kwa ushirikiano mzuri wenye manufaa katika seka ya afya nchini. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mambo ya nje ,kikanda na ushirikiano wa afrika mashariki wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano baina ya China na Tanzania yaliyofanyika Dar es Salaam. Dk.Mahiga aliwaeleza washiriki katika hafla hiyo kuwa   China ilionesha nia thabiti kuisadia Tanzania katika mambo mbalimbali baada yakupata Uhuru kutoka kwa wakoloni na mwaka 1968 nchi hizo mbili zilisaini hati ya makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya afya.   Amesema kuwa pamoja nakupokea misaada mbalimbali kutoka China ,Tanzania nayo ina mchango na msaada mkubwa kwa Taifa hilo linalo kadiriwa kuwa Taifa la pili kwa uchumi unaokuwa kwa haraka baada ya Marekani. “China imefanya mengi kwetu lakini katika sekta ya afya imetusaidia sana kwakuwapa madaktari wetu mafunzo huko china tokea kuanzishwa kwa mashirikiano haya ,hata sisi pia tunaisaidia China kwa

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekataa kuzindua stendi kuu mpya ya Mailmoja Kibaha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekataa kuzindua stendi kuu mpya ya Mailmoja Kibaha mkoani Pwani, akiwa katika ziara yake mkoani humo.  Hatua hiyo ameifikia kutokana na kupata wasiwasi wa utekelezaji wa mradi kuwa na baadhi ya mapungufu ambapo amedai baada ya kufanya uchunguzi wiki mbili ama tatu zijazo atakwenda kuuzindua. Akizungumza katika stand hiyo, Samia alieleza, kuna minong’ono wameisikia kuhusu mradi huo hivyo ni jukumu lake kuibeba na atakapo jiridhisha atarudi kwa mara nyingine .  Hata hivyo, alisema atakutana na mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mkuu wa mkoa kuzungumzia suala hilo. “Msishtuke kwa hili ni kawaida kwa kuchukua hatua za aina hii ili kujiridhisha kwa maslahi ya halmashauri, mkoa na watumiaji kijumla “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu na kusikia malalamiko ya wananchi, tumepata malalamiko kidogo kuhusu stand hii, serikali ni ya uwazi na ukweli hivyo sitofungua stendi “alisisitiza Samia.  Samia alimpo

Wananchi wa Mpwapwa wafanyiwa upimaji wa afya na utabibu

CHAMA cha madaktari nchini kwa kushirikiana na Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Shirikisho la Vyama Vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA)kimefanya kambi ya upimaji wa afya na utabibu kwa wananchi wa Mpwapwa. Akizungumza kwa njia ya simu jana kutoka mkoani humo Meneja Mradi wa Shirikisho la Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza(TANCDA) Happy Nchimbi alisema kuwa kambi hiyo ya upimaji wa afya ulianza Oktoba 21 na kumalizika (kesho) Oktoba 28 mwaka huu. Pichani ni Mhe Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam baada ya kupima afya yake,kutoka kushoto ni Rais wa chama cha madaktari Tanzania dr Obadia Yongole, TANCDA project manager Happy Nchimbi, waziri ofisi ya rais tamisemi mhe Selemani Jafo,muuguzi Anna Lamerk,Muuguzi Judith Adhiambo na mwisho ni dr Alexander Missungwa. Happy amesema kuwa katika kambi hiyo waliweza kutoa huduma ya upimaji Bure wa magonjwa yasiyoambukiza ambao umefanywa na wao TANCDA nakuwa umeweza kuwapima

CEO Apple Inc ashindwa kujutia kauli yake ya kuwa yeye ni shoga

CEO wa Kampuni maarufu duniani ya vifaa vya Elekroniki, Apple Inc, Tim Cook amesema kuwa hajutii kauli yake ya kutangaza hadharani kuwa yeye ni shoga aliyoitoa miaka minne iliyopita. Tim Cook Akihojiwa na CNN, Cook amesema yeye kuwa shoga ndio zawadi ya kipekee aliyopewa na Mungu, na alijitangaza hivyo ili kuwapa sauti watu wengine ambao wanapenda aina hiyo ya mapenzi. “ Najivunia sana kuwa hivi, ” amemwambia mtangazaji wa CNN Christiane Amanpour “ nadhani hii ndio zawadi pekee niliyopewa na Mungu “. Bilionea huyo mwezi Oktoba 30, 2014 alijitokeza hadharani na kutangaza kuwa yeye ni shoga jambo ambalo lilizua mijadala duniani. “ Nilichukua uamuzi wa kutangaza hadharani baada ya kuona barua pepe za watu wengi wakiniulizia kama mimi ni shoga, pia nimewapa sauti hata wale watu ambao hawana sauti lakini wameumbwa hivyo, “amesema Cook. Cook anakadiliwa kuwa na utajiri wa dola milioni $785 ambazo ni sawa na Trilioni 1.7 za Kitanzania.

Serikali yaanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono nchini

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo ameitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii. Wema Sepetu Akiongea na kituo cha runinga cha EATV, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni. Kwa upande mwingine, Mhe. Shonza amesema kuwa licha ya wasanii hao kuhojiwa na Bodi ya  filamu pia watahojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

WAZIRI MKUU NCHINI APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti ya uchunguzi wa  ajali ya kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kuchunguza ajali hiyo. Amepokea ripoti hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 25, 2018) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara,kwenye makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuishikuru kamati hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo imethibitisha umakini wao. Pia ameipongeza kamati hiyo kwa namna walivyotumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya mambo waliyoyabaini. “Nimepokea taarifa kwa niaba ya Serikali, Serikali itafanya mapitio ya taarifa yote na viambatisho vyake na itapitia kwa kina mapendekezo mliyoyatoa ambayo yote yatafanyiwa kazi.” Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaamini mambo yote yaliyosheheni katika taarifa hiyo ni yale ambayo Watanzania wanasu