CHAMA cha madaktari nchini kwa kushirikiana na Wilaya ya Mpwapwa
pamoja na Shirikisho la Vyama Vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza
Tanzania (TANCDA)kimefanya kambi ya upimaji wa afya na utabibu
kwa wananchi wa Mpwapwa.
Akizungumza kwa njia ya simu jana kutoka mkoani humo Meneja Mradi
wa Shirikisho la Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza(TANCDA) Happy Nchimbi
alisema kuwa kambi hiyo ya upimaji wa afya ulianza Oktoba 21 na
kumalizika (kesho) Oktoba 28 mwaka huu.
Pichani ni Mhe Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam
baada ya kupima afya yake,kutoka kushoto ni Rais wa chama
cha madaktari Tanzania dr Obadia Yongole, TANCDA project
manager Happy Nchimbi, waziri ofisi ya rais tamisemi mhe
Selemani Jafo,muuguzi Anna Lamerk,Muuguzi Judith Adhiambo
na mwisho ni dr Alexander Missungwa.
baada ya kupima afya yake,kutoka kushoto ni Rais wa chama
cha madaktari Tanzania dr Obadia Yongole, TANCDA project
manager Happy Nchimbi, waziri ofisi ya rais tamisemi mhe
Selemani Jafo,muuguzi Anna Lamerk,Muuguzi Judith Adhiambo
na mwisho ni dr Alexander Missungwa.
Happy amesema kuwa katika kambi hiyo waliweza kutoa huduma ya upimaji
Bure wa magonjwa yasiyoambukiza ambao umefanywa na wao TANCDA
nakuwa umeweza kuwapima wananchi zaidi ya 1500 ambapo wanachi
waliendelea kujitokeza kupata huduma hiyo.
Picha ya pili Selemani Jafo,waziri wa nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi akiwa anachekiwa kiwango cha sukari kwenye damu na
muuguzi Sister Anna Lameck na pembeni ni sister Judith Adhiambo.
Tamisemi akiwa anachekiwa kiwango cha sukari kwenye damu na
muuguzi Sister Anna Lameck na pembeni ni sister Judith Adhiambo.
"Wananchi wamefurahi sana na huduma hiyo ambapo wengi wao walikuwa
na tatizo la shinikizo la damu bila wao wenyewe kujifahamu,lakini
pia wengi wamegundulika kuwa na uzito wa juu,"amesema Happy.
Happy alisema wananchi wa Mpwapwa wanahitaji sana elimu ya magonjwa
yasiyo ya kuambukiza na visababishi vyake hasa ulaji unaofaa,ufanyaji
mazoezi na kupunguza matumizi ya pombe kwa wingi.
Aidha amesema kuwa katika zoezi hilo waziri wa nchi ofisi ya TAMISEMI
ndiye alikuwa mgeni rasmi na alijionea zoezi hilo likiendelea,
na kuona uhitaji wake kwa wananchi.
Aliongeza kusema kuwa huduma za upasuaji mbalimbali zilitolewa, na
madakari bingwa wa magonjwa ya watoto, kina mama, mifupa, pua,maskio,
macho pamoja na magonjwa ya ndani, upimaji wa virusi vya ukimwi na
pia kulikuwa na uchangiaji wa damu na wataalumu wa dawa za
usingizi pia walikuwepo.
Meneja huyo alisema upasuaji zaidi ya 100 ulifanyika ambapo wananchi
wengi wamepata faraja sana.
Comments