Serikali yaanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono nchini
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo ameitwa kuhojiwa na
Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha
kwenye mitandao ya kijamii.
Akiongea
na kituo cha runinga cha EATV, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na
Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema wameanza kuwachukulia hatua wasanii
wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni.
Kwa
upande mwingine, Mhe. Shonza amesema kuwa licha ya wasanii hao kuhojiwa
na Bodi ya filamu pia watahojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA).
Comments