WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na
Mazingira January Makamba ,amewataka watanzania
kutumia fursa za mazingira kama chanzo cha kuwainua kiuchumi.
kutumia fursa za mazingira kama chanzo cha kuwainua kiuchumi.
Mhe. Makamba amesema kuwa changamoto za mazingira
zikitumika vyema zitaweza kutengeneza fursa nyingi za katika
kaya na jamii.
Amesema kuwa serikali imekuwa na harakati sahihi katika
kutatua vikwanzo kwa wajasiriamali ambao wamewekeza
kupitia mazingira ili kuhakikisha wanakuwa katika mazingira
mazuri.
"Bado tunaendelea kutumia mbinu mbalimbali za kuhakikisha
wananchi wanapata fursa za kiuchumi ambazo zinaondoa kero
ya uchafuzi wa mazingira,"amesema Makamba.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga vema
kuaendelea na mipango ya kuzuia mifuko ya plastic ambapo
sasa wamesitisha utoa vibali kwa kiwanda kinachotaka
kuzalisha mifuko hiyo a nchini kwa kuwa imeonekana
inachafua mazingira.
Wakichangia mkakati huo wadau wa mazingira jijini Dar es
Salaam wamesema kuwa ili kufikia malengo serikali inapaswa
kutoa ushirikiano kwa wajasiriamali wadago ambao mlengo
wao tayari umeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya
mazingira.
Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira Duniani
(UNEP) Joyce Msuya, akichangia mada kwenye maonyesho ya
mjadala huo kuhusu fursa za kiuchumi katika mazingira,
ameweza kutoa ushauri na kusaidia kutatua changamoto za
mazingira.
Msuya amesema kuwa ili kufikia malengo inapaswa
kubadilisha wataalamu jambo ambalo litasaidia kuboresha
utendaji katika kupata fursa za kiuchumi kupitia changamoto
za mazingira.
Comments