Vodacom katika kuhakikisha wanafikia wateja wao wote popote walipo, wamefungua duka katika wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Bw Lengai Ole Sabaya
akisaini kitabu cha kumbukumbu baada ya kuzindua duka la Vodacom
Tanzania wilayani hapo jana. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Vodacom Tanzania
Kanda ya Kazkazini, Brigita Steven na Mkuu wa duka hilo, Bi Agripina
Boisafi (wa kwanza kushoto) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Bw. Lengai Ole Sabaya akizindua rasmi duka la Vodacom Tanzania jana wilayani
hapo ikiwa ni mpango wa kuhahakikisha wanafikia wateja wao wote, popote
walipo. Kando yake ni Agripina Boisafi, Mkuu wa Duka hilo.
Comments