Nyota wa Kitanzania ambaye anakipiga ligi ya Ubelgiji kupitia klabu ya Genk, Mbwana Samatta amefunga goli 2 na kutoa Assist 1 katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Besiktas ugenini katika Europa League.
Kufikia sasa Genk imefunga mabao 7 na kuruhusu matano. Samatta amecheza mechi 8 za Europa na kufunga mabao 9 katika hatua ya makundi na kufuzu .
Katika hatua ya Makundi Samatta ana mabao matatu kwenye mechi 3.
Kufikia hivi sasa Samatta amehusika katika magoli 11 katika michezo 8, magoli 9 na asisst 2 .
Takwimu za jumla za Samatta msimu huu amehusika magoli 18 kwenye michezo 18 ambapo magoli 16 na assists 2.
Mpaka sasa Samatta amehusika mabao 63 katika michezo 130, mabao 50 na Asissts 13.
Comments