Inaelezwa kuwa katika nchinyingi zinazoendelea wasichana hawanauhuruwa
kutumia simu za mkononi kamailivyokwa wavulana,Wasichana wanaazima
nakupigianasimu kwasiri jamboambalo linawawekakatikahatarikubwa.
Utafitihuo uliofanywa na MIT D-Lab, unadadisi hali hatarishi itokanayo na
wasichanakukosa uhuruwakutumiasimu za mkononi katika nchi 25
zikiwemoindia,Tanzania, Afrika ya Kusini, Nigeria na Bangladesh.
Kecia Bertermann ambaye ni Mkurugenzi wa ufundi na Utafiti wa kidijitali,
Girl Effect, alisema kuwa Utafiti huu unaonyesha ukweli wa hali halisi
ya wasichana walivyo nyuma kwenye foleni ya kupata simu. Hii ina maana
wasichana hupata matatizo zaidi na manufaa kidogo kama yapo; bila
kupewa muda au idhini ya kujiamini kudadisi matumizi makubwa zaidi ya
simu elimu na ujuzi wa kiteknolojia wa wasichana hudumazwa.
Amesema upatikanaji sawa wa teknolojia ni eneo la utafiti lenye kukua,
lakini 'wasichana' hupatikana mara kwa mara ndani ya jamii kubwa ya
'wanawake' na hivyo changamoto ambazo ni mahususi kwao huwa haziripotiwi.
"kwa kuwa wasichana wengine wanaamua kutumia simu kwa siri,wanaweza
kuogopa kutoa taarifa kwa wazazi au marafiki pale ambapo kuna jambo
hatarishi,na hivyo kujiweka kwenye hatari kubwa zaidi."Amesema Kecia
Bertermann.
Aliongeza kusema kuwa Matokeo yake, wasichana wanaona hofu ya wazazi
juu ya usalama wao ndio kizuizi kikuu kwaokupata simu asilimia 47,ambapo
wavulana wanasema gharama ndio kizuizi kikubwa zaidi asilimia 60.
October 11 mwaka huu sikuyabinti,Asasiisiyoyakibiashara yaGirl Effect
ikishirikiana na Vodafone Foundation imechapisha matokeo ya utafiti wa
kwanza wa kimataifa juu ya jinsi wasichana wadogo wanavyopata na kutumia
teknolojia ya simu.
Utafiti unaonesha kwamba wavulana wana uwezekano wa kuwa na simu mara
1.5 zaidi kuliko wasichana, na kuwa na uwezekano wa kuwa na simu janja
(Smart phone) mara 1.3 zaidi,kutokana na upendeleo wa kijamii na
vikwazo vingine vyenye kuzuia matumizi ya simu kwa wasichana.
Uhuru wa kutumia simu za mkononi kwa wasichana walio katika nchi zina
zoendelea ni mdogo kuliko inavyotarajiwa; wakati 44% tu ya wasichana
waliohojiwa katika utafiti walisema wanamiliki simu, zaidi ya nusu (52%)
walisema wanapata simu kwa kuazima.
Hata hivyo, utafiti unaonesha kwamba simu zinafanya wasichana kujisikia
kutotengwa(50%),kuwa na uhuru wa kupata elimu (47%), kujiburudisha
(62%), kuwafunulia habari zilizofichika(26%), na kuwafanya wajiamini (20%).
Hata hivyo, utafiti huu – wa ubora na uwiano, uliofanyika katika nchi 25 -
umegundua kuwa uhuru wa matumizi ya simu kwa wasichana unadhibitiwa kwa
kiasi kikubwa na mazoea ya kijamii ambayo huwazuia kuwa na uhuru sawa na
wavulana. Zaidi ya theluthi mbili (67%) ya wavulana waliohusishwa kwenye
utafiti waliripoti kuwa na simu (ikilinganishwa na 44% ya wasichana) na 28%
wakisema waliazima - ikilinganishwa na zaidi ya nusu (52%) kwa wasichana.
Aidha inaelezwa katika nchi kama Nigeria, Malawi na Tanzania, wavulana wana
uwezekano mkubwa wa kutumia simu kwa shughuli nyingi zaidi kama Whatsapp
na Facebook, kutafuta habari kwa mtandao, au kutafuta kazikuliko wasichana.
Katika maeneo haya, wasichana, kwa upande mwingine, hutumia simu kwa kazi za
kawaida zenye kuhitaji ujuzi na ufahamu mdogo sana, mathalan kuwapigiawazazi
wao au kutumia kikokoteo.
Comments