Katika kuadhimisha miaka 18 ya utoaji huduma kwa wateja
wao Vodacom Tanzania (PLC)yafanyamwezimzimawa October kuwa mwezi wa huduma kwa wateja.
Vodacom, imeendeleza sherehe za wiki ya huduma kwa wateja,ambazo
huadhimishwa wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, na mwaka huu kaulimbiu
ikiwani ‘Kusherehekea ubora wa utoaji huduma’.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa kampuni ya
Vodacom Tanzania, Bi. Harriet Lwakatare, amebainisha kuwa,lengo
kuu la kuendeleza maadhimisho hayo ni kuwashukuru wateja wao, watoa huduma na kuonyesha
huduma mbalimbali wanazozindua kwa dhumuni la kuwasaidia wateja.
“Tunafurahia kuona Vodacom inaongoza katika kubadilisha
maisha ya Watanzania zaidi ya milioni 12 na kuwaunganisha popote duniani. Hudumazetu
zimekuwa za kwanza nchini, zimepokelewa vizuri na kuendelea kutufanya Mtandao
bora wa simu nchini.”
Akiongelea mchango wa hudumazao kwa watanzania na uchumi
kwaujumla, Harriet alisema kuwa“MPesa imekuwa msaada mkubwa kwa huduma zakifedha
kama kutuma na kupokea fedha ndani na nje ya nchi, kufanyamanunuzi, na kulipa bidhaa
na ankara”. Huduma nyongeza kama M-Pawa imesaidia kuboresha maisha ya watu daraja
la chini na hata wakati kwa kutoa mikopo isiyo na usumbufu kwa riba nafuu.
Akitoa ufafanuzi kuhusu mageuzi yanayo ongezaubora wa
huduma, kiongozi huyo anasema kaziyao hukamilika pale wanapo hakikisha changamoto
au tatizo la mteja limetatuliwa na sihivyo tu,balinamteja amekiri kuridhika na utatuzi
huo.
Vodacom, ijulikanayokama ‘mtandaosupa’ inajivunia kuwaunganisha
ndugu, jamaa na marafiki kuwana mtandao uliosambaa nchi nzima na kutoa intaneti
yenye kasi zaidi. “Tuna mfikiria mteja wetu na kumfanya kuwa kiini cha kila ubunifu
tunaouzindua.
Hatuishii hapo
tu bali, tunaendelea kusikiliza na kuchukua maoni ya wateja wetu kwa ajiliya maboresho
zaidi”.
Kuhusu kauli mbiu ya mtandao huo, ‘Yajayo Yanafurahisha’
Lwakatare amesema kwamba ,kaulihii imelenga kuonyesha Vodacom imejidhatiti kuboresha
huduma kwa wateja wao kupitia njia za kidigitali zaidi ambazo wateja wanapata msaada
wapapo kwa hapo kwa kuchati moja kwa moja (Live chat) na watoa huduma.
Kadhalika,Lwakatare anabainisha kuwa kupitia mitandao
ya kijamii Facebook, Instagram, na Twitter wana kitengo maalum chenye ueledi wa
kutosha kumsaidia mteja kupata taarifa na ufumbuzi wa matatizo mbalimbali kwa haraka.
Piakupitiamaoniyanayotolewawakatiwatejawanapakuwa application
zetukwenye ‘Google play’ au ‘App Store’, Vodacom imehakikisha maoni yao yana fanyiwa kazi na kupatiwa
majibu papohapo.
Lwakatare pia amethibitisha Vodacom inaendelea kusogeza
zaidi huduma kwa wateja kupitia maduka yao ya liyozaidi ya 400 nchini.
Kuhusiana na kutoa elimu kwa wateja kuhusu wimbi la
matapeli ambao hutumia fursaya M-Pesa kuibiawateja fedha, Harriet anasema
Vodacom kwa sasa inakampeni mahususi ya kuelimisha wateja.
Mara kwa mara, watumiaji wa simu za mkononi wamekuwa
wakilalamika kupokea ujumbe mfupiwamaneno au kupigiwasimu wakielezwakuwa wameshinda,
kabla ya kupewa zawadi matapelihao huwataka watume kiasi fulani cha pesa.
Watumiajiwasimu wanatakiwa kuwa makini pindi wanapopigiwasimu
hasa na watu wasio wafahamu na pia kulinda na kutokutoa namba ya siri wala taarifa
zinazohusu akaunti za fedhazao kwa mtumwingine.
“Tunapendakuwajulisha wateja kuwa na mbayetu inayotumika
kuwasiliana na wateja wanaoshinda promosheni zetu au wanaohitajika kwanamnayoyote,
huwa ni namba0754 100 100 nasivinginevyo,” Harriet anabainisha.
Kuhusiana na namna Vodacom ilivyoboresha usalama wa mteja
katika utumiaji wa huduma ya M Pesa, Lwakatare amethibitisha usalama wa miamala
ya wateja wao nakuwa hakikishia wateja wao kuwa M-Pesa imethibitishwa na kampuni
ya kimataifa ya GSMA kwa usalama wake nahudumu bora zaidi.
Changamoto nyingine inayoripotiwa na wateja ni miamala
inayo tumwa kimakosa, na Lwakatare amebainisha uwezekano wa wateja kuweza kurudishamiamala
inayotumwa kimakosa punde wanapogundua wamekamilisha muamala usio sahihi.
Vodacom inaendeleakuboresha huduma kwa kuzindua mifumo
ya kulipia bidhaa kwenye mitandao kama Amazoni, Ebay, Easybuy kidigitali
kwa kutumia M-Pesa Mastercard ikiwani mpango wa kuhakikisha huduma zao zinawagusa
watu katika sekta zote. Mkurugenzi huyo amemaliza mwezi huu kwa kuwashukuru wateja
wao na kuwataka waendelee kutumia mtandao huo kwani hakika, yajayo,
yanafurahisha!
Comments