Rais wa Rwanda Paul
Kagame
Rais wa Rwanda Paul
Kagame amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri na
kumteua Dkt Richard Sezibera kuwa waziri mpya wa mashauri ya nchi za
nje.
Jenerali James Kabarebe aliyekuwa mtu wa karibu sana na Rais
Kagame amepoteza wadhifa wake kama waziri wa ulinzi na badala yake
akateuliwa mshauri wa rais katika masuala ya usalama.
Katika
mabadiliko makubwa na ya kushtukiza aliyofanya Rais Kagame wizara 8
kati ya 23 zimepata mawaziri wapya zikiwemo wizara nyeti tatu, wizara
ya ulinzi ambayo sasa inaongozwa na Meja jenerali Albert Murasira
aliyechukua nafasi ya Jenerali James Kabarebe.
Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema si wengi walitarajia mabadiliko haya.
Jenerali
Kabarebe ambaye amepewa nafasi ya kuwa mshauri maalumu wa rais wa
maswala ya ulinzi na jeshi alikuwa mshirika wa karibu sana na Rais Paul
Kagame tangu vita vilivyong'oa utawala wa rais Juvenali Habyarimana
miaka ya 1990.
Tangu RPF kushika hatamu akachukua nyadhifa nyeti za utawala wa jeshi.
Comments