Baada ya kupokea kipigo cha mabao mawili kutoka kwa nahodha wa
Tanzania, Mbwana Samatta kwenye mchezo uliyomalizika kwa 4 – 2
mlindalango Loris Karius sasa kurejeshwa Liverpool.
Klabu
ya Besiktas imenuia kumrejesha kipa huyo, Karius ambaye yupo hapo kwa
mkopo wa miaka miwili akitokea Liverpool na badala yake wakimhitaji
Divock Origi.
Miamba hiyo ya Uturuki imeripotiwa kuwa imechoshwa
na huduma yake na hivyo tayari imefanya mazungumzo na Liverpool kuona
namna ya kumrejesha ili kubadilishana na Divock Origi.
Karius
ambaye ameonekana kutokuwa na matokeo mazuri toka kutua kwake ndani ya
klabu ya Besiktas haswa matokeo mabovu ya Europa League dhidi ya KRC
Genk ambapo alikubali kipigo cha mabao 4 – 1 huku mshambuliaji hatari wa
Tanzania Mbwana Samatta akiweka kimyani mabao mawili atarejea Anfield
mwakani mwezi Januari.
Mlindalango huyo raia wa Ujerumani yupo
kwenye miamba hiyo ya soka ya Uturuki kwa mkopo wa miaka miwili ambayo
timu hiyo amepewa nafasi ya kumnunua moja kwa moja baada uwepo wake kwa
mkopo ukimalizika.
Karius anakumbukwa zaidi baada ya kuizawadia
Real Madrid jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa
fainali wa Champions League ambapo mashabiki wengi wa majogoo hao wa
England wakimtupia lawama kwa kukubali kufungwa mabao mepesi.
Comments