kujiunga na benki hiyo kwa kuwa uchumi wake umekuwa
ukizidi kuimarika nakuwataka wananchi kuendelea kuiamini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa
idara ya fedha ya benki hiyo James Ngahio wakati akitangaza
faida ya shilingi bilioni 1.4 katika kipindi cha robo ya tatu
ya mwaka 2018.
“Benki nyingi zimeyumba lakini sisi, tunamshukuru Mungu
tunaendelea vizuri pamoja na changamoto za kiuchumi,
kupitia faida hii ni dhahiri kuwa tupo vizuri wananchi
waendelee kutuamini,”amesema
Ngahio alisema faida hiyo iliyopatikana katika kipindi
kinachoishia mwezi septemba mwaka huu, imeipiku hasara
ya shilingi bilioni 1.6 iliyopatikana kipindi kama hicho
mwaka 2017 ambayo inawakilisha ongezeko la asilimia 187.
“Benki imefanya juhudi za makusudi kuhakikisha inatoka
kwenye hasara iliyopata mwaka jana na kurudi kwenye faida,
baadhi ya hatua tulizo chukuwa nikuboresha mfumo wa
uedeshaji Biashara,"amesema.
Mfumo huo unahusisha gharama za uendeshaji ambazo zimeshuka,
kwakupunguza matawi hapa Dar es Salaam na kuanzishwa kwa
huduma mpya za kidijitali ambayo imevutia wateja wengi
ambao wameshawishika kufungua akaunti.
Naye Mkurugenza wa Biashara wa DCB Zacharia Kapama alisema
ukuaji wa faida umechagizwa na ukuaji wa mikopo ghafi ya
wateja kutoka shilinghi bilioni 89.3 mwezi septemba 2017
hadi sh bilioni 91.3 mwezi septemba mwaka huu.
“Kufuatia ukuaji huo ukuaji wa mikpo ya jumla ya sh bilioni 50
imetolewa kwa wakopaji hadi kufikia septemba 2018 na idadi ya
wateja wetu imeongezeka kutoka 144,445 mwezi desemaba 2017
hadi kufikia wateja 157,366 kwa mwezi septemba 2028,”amesema
Pamoja na ongezeko la mikopo ghafi benki imefanikiwa kupunguza
kiwango cha mikopo chefuchefu kutoka asilimia 18.9 desemba 2017
nakufikia asilimia 17.8 septemba 2018.
Benki ya DCB ilianzishwa 2008 ikiwa kama benki ya jumuiya ya
wananchi wa Dar es Salaam na mwaka 2008 ilifanywa na manispaa
ya jiji la Dar es Salaam hadi mwishoni mwa septemba 2018 imeweza
kutoa mikopo ya shilingi bilioni 150.
Comments