Serikali ya Tanzania imeipongeza serikali ya
watu wa china kwa ushirikiano mzuri wenye manufaa katika seka ya afya nchini.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mambo ya nje ,kikanda na
ushirikiano wa afrika mashariki wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya
ushirikiano baina ya China na Tanzania yaliyofanyika Dar es Salaam.
Dk.Mahiga aliwaeleza washiriki katika hafla hiyo kuwa China ilionesha nia thabiti kuisadia Tanzania
katika mambo mbalimbali baada yakupata Uhuru kutoka kwa wakoloni na mwaka 1968
nchi hizo mbili zilisaini hati ya makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya
afya.
Amesema kuwa pamoja
nakupokea misaada mbalimbali kutoka China ,Tanzania nayo ina mchango na msaada
mkubwa kwa Taifa hilo linalo kadiriwa kuwa Taifa la pili kwa uchumi unaokuwa
kwa haraka baada ya Marekani.
“China imefanya mengi kwetu lakini katika sekta ya afya
imetusaidia sana kwakuwapa madaktari wetu mafunzo huko china tokea kuanzishwa
kwa mashirikiano haya ,hata sisi pia tunaisaidia China kwa mambo mengi,1974
wakati kura ya VETO ya Umoja wa Mataifa Mwalimu Nyerere alihamasisha wa afrika
kupigia kura China kuwa mjumbe kudumu wa baraza la usalama la UN,”amesema
Naye Balozi wa China Tanzania Wang Ke alisema kuwa hadi sasa
China imeleta madaktari 53 ambapo 11 walikula kiapo jana cha kuhudumu katika
hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Muhimbi,hospital ya rufaa ya Mbeya na
Taasis ya Moyo ya Jakaya Kikwete watakao hudumu zaidi katika magonjwa yasiyo
yakuambukizwa.
kuanzishwa kwa mashirikiano hayo madaktari 1,470 wamehuduma
Tanzania pamoja na changamoto mbalimbali hadi sasa jumla ya wagonjwa 300,000
wametibiwa na madaktari hao ,Balozi huyo amesema kuwa China itaendelea
kushirikiana na Tanzania kutoa huduma.
“Malengo yetu ni kuokoa maisha ya ndugu zetu watanzania na
tumeanza kuwafikia watu wa vijijini zaidi ambapo madaktari wetu wanatoa huduma
katika mikoa mbalimbali kama Mtwara, Mara, Kigoma na Mbeya na tunaendelea
kupanua huduma ya afya iwafikie wananchi wengi kadri iwezekanavyo,”amesema
Kwa upande wake Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema
kuwa watahakikisha ushirikiano huo unaendelea baina ya nchi hizo mbili kwakuwa
una manufaa kwa maisha ya watanzania.
“Tutaendelea kushirikiana na ndugu zetu wa china katika sekta
ya afya ili tuokoe maisha watanzania wengi kwakutoa huduma za kitabibu hapa
nchi nakuepuka kuwasafirisha wagonjwa wetu nje nchi kwa ajili ya
matibu,”amesema
Waziri Ummy ameongeza
kuwa dhamira kubwa ya serikali kwa sasa nikuboresha mazingira ya afya
nchini kwa kusomesha madaktari wengi lakini aliongeza kuwa wahandisi wa vifaa
vya afya nao ni muhimu sana.
Alisema kuanzishwa kwa mashirikiano hayo China imeshirikiana
katika mambo mbalimbali kiuchumi,kisiasa na kijamii, ambapo china imekuwa
mstari wa mbele sana katika matukio mbalimbali ya kijamii yakiwemo mafuriko na
maafa mbalimbali.
Comments