Wadau mbalimbali wakiwa katika Mkutano leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya
mkemia mkuuu wa Serikali Dkt. Fidelince Mafumiko akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imewataka wadau mbalimbali hapa
nchini kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha wanaleta ufanisi
katika kutekeleza majukumu yao.
Wadau hao ni Shirika la Viwango (TBS), Mawakala ya Maabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali (GCLA) pamoja na Chama cha Mawakala wa forodha
Tanzania (TAFFA) ambao wamekutana leo kwa ajili ya kujadili taratibu za
uingizaji wa bidhaa hapa nchini
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha
wadau mbalimbali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Agnes Kijo, amesema kuwa
mkutano umelenga kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika
utendaji.
Agnes amesema kuwa mkutano ni muhimu kutokana kila mdau amepata fursa
ya kueleza majukumu yake katika utendaji pamoja na kuangalia matakwa ya
kisheria ambayo imekuwa ikitumika.
"Uwepo wa mkutano huu kwetu TFDA ni jambo jema kutokana majukumu yetu
ni kuaangalia usalama wa chakula kutokana na bidhaa zinazoingizwa hapa
nchini" amesema Agnes.
Amesema kuwa ni vizuri kuaangalia kila jambo liwe linakwenda vyema
katika kufanikisha maendeleo katika kuzuia bidhaa feki ambazo zimekuwa
zikiingia hapa nchini kinyume na sheria.
Agnes amefafanua kuwa taasisi zote ambazo zimeshiriki mkutano huo
zina nia ya kujirekebisha ili kuhakikisha kila mmoja nafanya kazi yake
kikamilifu.
"Kumekuwa sitofahamu utaratibu wa kuingiza bidhaa kwani watu wa
forodha wamekuwa wakichelewa kutoa mizigo kutokana na baadhi ya
wafanyabiashara kuchelewa kuomba kwa vibali" amesema Agnes.
Hata hivyo ameeleza kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kukusanya kero
za wadau mbalimbali na kuzifanyia kazi jambo ambalo linaweza kuleta
ufanisi katika utendaji.
Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya mkemia mkuuu wa Serikali Dkt.
Fidelince Mafumiko, amesema kuwa mkutano huo utawapa fursa ya kupata
mrejesho katika huduma wanazotoa taasisi mbalimbali.
Dkt. Mafumiko amesema kuwa ni mwanzo mkubwa mzuri katika kutengeneza mipango ya kuendelea kutoa huduma bora.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Viwango (TBS) Lazaro Msasalaga,
amesema kuwa mkutano utasaidia kuongeza ufanisi katika mpango wa utoaji
wa mizigo kwa kutatua changamoto zinazotukabili katika taasisi.
"Tumekutana na Mawakala wa forodha katika kuangalia changamoto ambazo zipo ili zifanyiwe kazi" amesema Msasalaga.
Comments