CEO wa Kampuni maarufu duniani ya vifaa vya Elekroniki, Apple Inc,
Tim Cook amesema kuwa hajutii kauli yake ya kutangaza hadharani kuwa
yeye ni shoga aliyoitoa miaka minne iliyopita.
Akihojiwa
na CNN, Cook amesema yeye kuwa shoga ndio zawadi ya kipekee aliyopewa
na Mungu, na alijitangaza hivyo ili kuwapa sauti watu wengine ambao
wanapenda aina hiyo ya mapenzi.
“Najivunia sana kuwa hivi,” amemwambia mtangazaji wa CNN Christiane Amanpour “nadhani hii ndio zawadi pekee niliyopewa na Mungu“.
Bilionea huyo mwezi Oktoba 30, 2014 alijitokeza hadharani na kutangaza kuwa yeye ni shoga jambo ambalo lilizua mijadala duniani.
“Nilichukua
uamuzi wa kutangaza hadharani baada ya kuona barua pepe za watu wengi
wakiniulizia kama mimi ni shoga, pia nimewapa sauti hata wale watu ambao
hawana sauti lakini wameumbwa hivyo,“amesema Cook.
Cook anakadiliwa kuwa na utajiri wa dola milioni $785 ambazo ni sawa na Trilioni 1.7 za Kitanzania.
Comments