Skip to main content

Dkt Tizeba siku ya Chakula Duniani

Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (Mb) akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Leo tarehe 16 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal,WK)
Kikundi cha ngoma ya asili cha Mkoani Songwe kikitumbuiza mara baada ya waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (Mb) kuwasili kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Leo tarehe 16 Octoba 2018.
Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (Mb) akitoa salamu za Rais John Pombe Magufulu wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Leo tarehe 16 Octoba 2018.
Sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba ya waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (Mb) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Leo tarehe 16 Octoba 2018.

Na Mathias Canal-WK, Tunduma-Songwe

Tanzania imeendelea kuwa ghala la chakula kwa nchi za jirani kwa kipindi kirefu baada ya kujitosheleza kwa chakula takribani kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo. 

Tanzania imeweza kuuza ziada ya mazao mbalimbali ya chakula katika nchi za nje. Kulingana na takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kipindi cha mwezi Juni 2017 hadi Juni 2018 yameuzwa mahindi kiasi cha Tani 64,477.95  zenye thamani ya Shillingi Billioni 90.6  za kitanzania na maharage  Tani 99,434.45 zenye thamani ya shillingi Bilioni 222.0 za Kitanzania. 

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba (Mb),  tarehe 16 Octoba 2018 wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.

Dkt Tizeba alisema kuwa mazao hayo yamekuwa yakiuzwa zaidi katika nchi za Kenya, Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini na Uarabuni. 

"Pamoja na kuuza mazao nje ya nchi, nchi yetu imekuwa ikitegemea kuagiza zao la ngano kutoka nje ya nchi kutokana na uzalishaji mdogo wa zao hilo hapa nchini. Serikali inatoa wito kwa wakulima hususani wa maeneo ambayo zao hili linalimwa na kukua vizuri waweze kuongeza maeneo ya uzalishaji na tija ili nchi iweze kupunguza utegemezi wa zao hili kutoka nchi za nje" Alikaririwa akisema

Alisema, Pamoja na uzalishaji mzuri wa chakula nchini, Lishe duni (utapiamlo) kwa jamii na kwa baadhi ya maeneo inaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuathiri maendeleo ya wananchi kiafya, kielimu na kiuchumi.

Aidha, ili kuyafikia malengo endelevu ya maendeleo (Sustainable Development Goals), alisema , Lishe ni moja ya muhimili muhimu wa kuwezesha kufikiwa kwa malengo yote 17 hivyo Serikali kwa kulitambua hilo, imeamua kujumuisha masuala ya lishe kuwa mojawapo ya maeneo ya kimkakati katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. 

Kadhalila, aliwataka wadau wote wa lishe nchini kushiriki na kuonyesha bayana mchango wao katika kukabiliana na utapiamlo. 

Tarehe 16 ya mwezi Oktoba kila mwaka, Tanzania na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, huadhimisha Siku ya Chakula Duniani ambapo lengo la maadhimisho ya siku hiyo ni kukumbushana wajibu wa kila mmoja katika kupambana na njaa, kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa. 

Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu inayosema “ Matendo yetu ni hatima yetu. Dunia bila njaa ifikapo 2030 inawezekana”. "Kaulimbiu hii inatutaka kufanya kazi kwa umahiri mkubwa ili tujitosheleze kwa chakula na kuwa na akiba ya kutosha kuendesha maisha yetu ya kila siku." Alisisitiza Dkt Tizeba na kuongeza kuwa

"Pia kaulimbiu hii inatukumbusha kuacha kufanya mambo kwa mazoea na badala yake tutumie utalaamu katika kuongeza kuzalisha mazao  ya kilimo, mifugo na uvuvi."

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...