Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amekabidhi fedha tasilimu shilingi milioni 50 kama alivyoahidi kwaajili ya kusaidia maandalizi ya Taifa Stars kuelekea mchezo wake wa Kufuzu Afcon dhidi ya Lesotho utakaopigwa Novemba 18, 2018.
”Nawachangia milioni 50 ili iwasaidie katika maandalizi dhidi ya mechi yenu na Lesotho, muhakikishe zinatumika kwa watu wanaotakiwa kwenda” amesema Rais Magufuli.
Amesisitiza kuwa atafuatilia matumizi ya kile senti katika fedha hizo na watakaozitafuna watazitapika.
Aitaka Taifa Stars kuleta ushindi bila visingizio vyovyote akiwasihi wachezaji kuwa kitu kimoja, kuuchukulia mchezo huo kama vita na kupambana kwaajili ya taifa lao.
Comments