Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein amepongeza juhudi zinazochukuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) katika
kuendeleza miradi mbali mbali ya maendeleo na kueleza kuwa kuanzishwa
kwa “Program ya Pamoja ya Zanzibar” (ZIP) itakuwa ni kichocheo cha
mafanikio.
Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Mratibu mpya wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa eneo la Zanzibar Bi Dorothy Temu-Usiri.
Dk. Shein alieleza kuwa kutokana na uzoefu mkubwa wa utendaji kazi wa Mratibu huyo ana matumaini makubwa kuwa program hiyo sio tu itasaidia kuimarisha maendeleo ya Zanzibar bali itasaidia sana katika kufikia malengo ya maendeleo yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa (UN) hapa nchini.
Rais Dk. Shein alisema kwamba, malengo ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa Zanzibar yako wazi katika kila sekta na yanafahamika kwa wananchi wote wa Zanzibar jinsi yalivyolenga katika kuimarisha sekta za maendeleo.
Alisema kuwa (UN) imekuwa ikifanya kazi na kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali ikiwemo elimu, afya, upatikanaji wa maji safi na salama, utawala bora, uimarishaji wa haki za binaadamu, uwezeshaji, mapambano ya udhalilishaji wa kijinsia pamoja na uhifadhi wa mazingira.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) kwa mashirikiano inayotoa katika kuimarisha miradi mbali mbali ya maendeleo hapa Zanzibar hasa katika masuala ya wanawake na watoto.
“Programu ya Pamoja ya Zanzibar” (ZIP), inayohusisha Mashirika tisa ya UN, aliizindua Rais Dk. Shein hivi karibuni hapa Zanzibar ambapo katika uzinduzi huo alisisitiza haja kwa wafanyakazi kuleta mabadiliko ya fikra na mawazo na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuweza kuifanikisha progamu hiyo kwa ufanisi mkubwa.
Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein alimuhakikishia Mratibu huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na viongozi wake itaendelea kutoa mashrikiano makubwa kwa Umoja huo pamoja na viongozi wake wote wakiwemo wale wanaofanya kazi zao katika ofisi za Umoja huo hapa Zanzibar.
Alisisitiza kuwa Programu ya pamoja ni mradi wa kipekee unaolenga kuwawezesha watoto, vijana na wanawake hivyo ni matumaini yake makubwa kuwa malengo yaliokusudiwa yatafikiwa kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo.

Comments