Bingwa wa UFC, Khabib Nurmagomedov amesema kuwa yupo tayari kupigana na mwanamasumbwi Floyd Mayweather huku akihitaji pambano hilo lifanyike jijini Moscow.
Bingwa wa UFC raia wa Urusi, Khabib Nurmagomedov
Nurmagomedov raia wa Urusi ni mpiganaji anayetumia ‘martial artist’ anahitaji kupigana na Mayweather ambaye tayari alishampiga Conor McGregor katika pambano lililoingiza mkwanja mrefu.
Mpiganaji huyo anayegonga vichwa vya habari toka apate ushindi nbaada ya kumpiga McGregor jijini Las Vegas Oktoba 7 mwaka huu raundi ya nne, alipoulizwa kama yupo tayari kuzipiga na Mayweather amesema kuwa ni jambo linalowezekana.
Comments