Afisa Mtunzaji kumbukumbu Mwandamizi (Brela) Mwombeki Rutta amewataka
wataalam wa utunzaji kumbukumbu kujiunga katika chama cha watunza
kumbukumbu Tanzania (TARESO).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kupitisha rasimu ya katiba ya chama hicho, ambapo amesema kinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya kupitishwa kwa rasimu hiyo.
Amesema kuwa, Chama hicho kimekuwa kikifanya kazi nchi nzima kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo wahadhiri wa vyo vikuu, madaktari pamoja na wabobezi wa tasnia hiyo.
"Chama hiki ni Chama cha Tanzania nzima hivyo nawahamasisha wanataaluma ya utunzaji ambao hawajajiunga kujiunga nacho ili wapate Jukwaa huru la kusemea na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili "amesema Rutta.
Aidha amesema, Chama hicho kimejipanga vizuri katika kutatua changamoto za wanataaluma hao kwani kumekuwepo na vyama vingi vya kitaaluma katika Tasisi za Serekali na binafsi nchini lakini changamoto zimekuwa nyingi.
Ameongeza kuwa, wafanyakazi wa tasnia hiyo nchini waendelee kujiunga na chama hicho kwani uwepo wa chama hicho ni ukombozi katika tasnia hiyo kwa wanataatuma wote wa tasnia hiyo katika kupigania maslahi ya wanachama.
Hata hivyo amesema hadi sasa chama hicho kina wanachama zaidi ya 400 nchi nzima ambapo wamejipanga kukizindua hivi karibuni na kutumika kama jukwaa la wanataaluma kuhifadhi kumbukumbu.

Comments