Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2016

Kenya yaifuata Tanzania kuhusu bendera ya EAC

Baraza la mawaziri nchini kenya limeamrisha mara moja afisi za serikali na taasisi za umma kuanza kupeperusha na kutumia bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kucheza wimbo wa Afrika Mashariki. Agizo hili pia linazihusu shule zote nchini humo. Nchini Tanzania, tayari kuna agizo kwamba Bendera ya Taifa inafaa kupeperushwa ikifuatiwa na Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, vivyo hivyo Wimbo wa Taifa utaanza kupigwa ukifuatiwa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mwandishi wa BBC David Wafula amezungumza na Waziri wa Utalii nchini Kenya Najib Balala ambaye alikuwa katika kamati iliyofanya uamuzi nchini Kenya na kwanza alimwuliza, umuhimu wa hatua hii ni upi?

Kipa Juma Kaseja sasa kuinoa Timu ya Taifa ya Vijana

Kipa nyota nchini, Juma Kaseja ameteuliwa kuwa kocha wa makipa wa kikosi cha vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys. Kaseja anaungana na kikosi hicho ambacho kinasafiri kwenda kambini Madagascar kupitia Afrika Kusini. Kaseja amechukua nafasi ya kocha wa makipa aliyekuwepo awali ambaye anabaki nchini kwa ajili ya kushiriki kozi za ukocha. Kipa huyo wa zamani wa Simba, alikuwa katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na Mbeya City.

Klabi anayoichezea Mtanzania Mbwana Samatta yapata ushindi wa bao 1-0 kucheza Europa

Kikosi cha KRC Genk anachokichezea Mtanzania Mbwana Samatta kimepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cork. Ushindi huo ni katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Europa na sasa Genk iliyokuwa nyumbani itatakiwa kulinda ushindi huo finyu katika mechi ijayo ugenini. Shujaa wa Genk alikuwa ni Bailey ambaye alifunga bao hilo pekee huku Genk wakipoteza nafasi nyingi za kupata mabao zaidi.

Maelekezo ya Zitto Kabwe Kwa Wanachama wa ACT- Wazalendo Kuhusu Kauli ya Rais Magufuli Jana Singida

    Maelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC ) kwa wanachama wote wa ACT Wazalendo ( KC/01/2016 ). Tangu kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Utawala mpya umekuwa ukifanya kila juhudi kuminya uwezo wa Vyama vya Siasa kufanya Kazi zake kwa kisingizio kuwa huu ni wakati wa kufanya Kazi na kwamba Siasa zisubiri mwaka 2020. Chama chetu kilipinga kwa nguvu zote uzuiaji huu wa shughuli za kisiasa kwani ni kinyume cha Katiba ya Nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa, sheria namba 5 ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho Mara kwa Mara. Mnamo tarehe 5 Juni 2016 Chama chetu kilifanya Mkutano wa Hadhara Mbagala jijini Dar Es Salaam na kutangaza Operesheni Linda Demokrasia. Lengo la Operesheni hiyo ( Tamko la Mbagala 2016 ) ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa Nchi ya kidemokrasia na kuepuka mwelekeo wa Utawala wa Imla ambao ni utawala wa kidikteta. Chama chetu asili ya uundwaji wake ni kupinga tabia za kidikteta tulizokumbana nazo ndani ya Vyama tulivyokuwamo

Msome hapa Mohammed Dewji katika mpango wake wa kuinunua Timu Ya Simba

Kuelekea mkutano mkuu wa Simba unaotaraji kufanyika Jumapili ya Julai, 31, shabiki na mkeleketwa wa Simba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amezungumza mipango yake aliyopanga kuifanyia Simba kama akipata nafasi ya kununua hisa asilimia 51 za klabu hiyo. MO amesema kuwa mipango yake ni kuwekeza Bilioni 20 na amepanga bajeti ya klabu hiyo kwa mwaka iwe Bilioni 5.5, kiasi ambacho anaamini kuwa kitaweza kubadili mwelekeo wa Simba kutoka ilivyo sasa na kurudisha zama zake za kutwaa mataji ya ndani na kufika hatua nzuri kimataifa. MO alisema amefikia uamuzi wa kutaka kununua hisa katika klabu ya Simba kutokana na mapenzi aliyonayo katika klabu hiyo na hana nia yoyote ya kiabiashara na klabu hiyo kwani tayari ana biashara anazofanya ambazo zinam

kipigo cha Medeama:Pluijm kutoa ripoti

Kocha wa Mukuu ta klabu ya Yanga, Hans van Der Pluijm anatarajia kukabidhi kwa uongozi ripoti yake ya mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ambao walifungwa mabao 3-1. Yanga ilifungwa na Medeama, Jumanne wiki hii nchini Ghana na kuzima matumaini ya kucheza nusu fainali katika michuano hiyo kutoka Kundi A kwani ina pointi moja tu huku kinara TP Mazembe ikiwa na pointi 10. Inahitajika miujiza ili Yanga itinge nusu fainali kwani Medeama ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi tano sawa na MO Bejaia iliyopo nafasi ya tatu. Timu zote zimebakisha mechi mbili Ripoti hiyo ya Pluijm inatarajiwa kuwa na mambo mengi kwani juzi Alhamisi baada ya kuwasili nchini kutoka Ghana, aliwatupia lawama mabeki wake kwa kusema ndiyo chanzo cha kufungwa. Akizungumza na Championi Jumamosi, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Y

Mtandao wa umenunuliwa na kampuni ya Verizon kwa dola bilioni 5

Kampuni ya internet ya Marekani, Yahoo imenunuliwa na kampuni ya mawasiliano ya Verizon Communications kwa dola bilioni 5, fedha taslimu. Yahoo itaunganishwa na AOL, kampuni nyingine ya internet iliyopoteza umaarufu ambayo nayo ilinunuliwa mwaka jana na kampuni hiyo. Hata hivyo dili hilo halijumuishi hisa za thamani ilizonazo kwenye kampuni ya China, Alibaba. CEO wa Yahoo, Marissa Mayer Fedha hizo ni ndogo zaidi kuliko dola bilioni 44 ambazo kampuni ya Microsoft ilitaka kuinunua Yahoo mwaka 2008. Yahoo iligoma kununuliwa kwa kiasi hicho cha fedha. Enzi za umaarufu wake, Yahoo ilikuwa na thamani ya dola bilioni 125. CEO wa saba na wa mwisho wa Yahoo, Marissa Mayer, anadaiwa kuwa ataondoka baada ya dili hilo huku akilipwa kiinua mgongo cha dola milioni 50.

KWA SASA ARSENAL WANAHITAJI ZAIDI YA SANCHEZ NA OZIL-COLLYMORE

  Arsenal wanahitaji kufanya usajili zaidi kutokana na kukosa wachezaji wenye ubora wa juu huku Mesut Ozil, Alexis Sanchez na Granit Xhaka wakisemwa kwamba si wazuri kwa kiwango hicho, hii ni kwa mujibu wa Stan Collymore. Arsene Wenger amemsajili Xhaka pekee kwenye dirisha hili la usajili huku akisisitiza kwamba yuko tayari kutumia pesa kusajili isipokuwa kwa wachezaji sahihi tu kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Arsenal tayari wamewakosa Jamie Vardy huku Gonzalo Higuain akitajwa kuwa njiani kujiunga na Juventus, na hivyo basi, Collymore anahisi kwamba kuna uhitaji mkubwa wa klabu hiyo kufanya usajili wa maana zaidi ili kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa kwenye mbio za kuwania taji la ligi la msimu ujao. “Bado naamini kwamba timu hii ya Wenger itakuwa katika nafasi nne za juu endapo tu watasajili beki wa kati mzuri na mshambuliaji wa kati mzuri, vinginevyo sidhani kama watakuwa na fursa hiyo,” ameandika kwenye gazeti la Sunday Mirror. “Kwamba, kwa

Zitto na Maalim Seif waalikwa Democratic cha US

  Wanasiasa, Zitto Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad kwa pamoja wameitwa jijini Philadelphia, Marekani kwaajili ya kuhudhuria mkutano mkuu wa chama cha Democratic. Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo. Wanasiasa hao wameitwa kuhudhuria mkutano mkuu wa cha hicho utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa Marekani kupitia chama hicho. Marekani inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Novemba 8 mwaka huu ambapo Clinton atathibitishwa kwenye mkutano huo kuchuana na Donald Trump wa chama cha Republican. Akizungumza na gazeti la Mwanahalisi, Ofisa Habari wa ACT- Wazalendo, Abdallah Khamis, amesema, “wakati Zitto akiwa kwenye mkutano huo, atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani.” “Kufanya kikao cha maandalizi juu ya ufunguzi wa tawi la wanachama wa ACT Diaspora la nchini Marekani pamoja na kuwa na mazungumzo maalum na Maalim Seif

Simba yaendelea kujiweka vizuri na msumu ujao ya shusha straika kutoka Ghana

Sweetbert Lukonge na Hans Mloli WAKATI benchi la ufundi la timu ya Simba likiendelea kuwafanyia tathimini baadhi ya wachezaji wake wa kimataifa wanaofanya majaribio ya kutafuta nasafi ya kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao, uongozi wa klabu hiyo unatarajia kushusha straika mpya kutoka nchini Ghana. Kwa jinsi mipango ilivyo, straika huyo anatarajiwa kutua nchi leo au kesho na kwenda moja kwa moja mkoani Morogoro kuungana na kikosi cha timu hiyo kilichojichimbia huko kwa ajili ya maandalizi yake ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20, mwaka huu. Atakapofika huko, straika huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mpaka tunaenda mitamboni, atafanyiwa majaribio na Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog ambaye anaendelea na harakati zake za kukisuka upya kikosi hicho. Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa ujio wa straika huyo klabuni hapo umetokana na uongozi wa klabu hiyo kufanyiwa mipango

nyota wa bongoflava atangaza kujenga Africa Kusini

kama ulikuwa kwenye mtandao wa Instagram na umebahatika kumfollow Diamond Platnumz tu bila kumfollow Zari basi story hii inaweza kuwa mpya sana kwako. Lakini kama pia ume m follow Zari na huna time ya kusoma comment pia story hii itakuwa imekupita. Issue nzima ilikuwa kwa upande wa Zari ambapo siku ya jana alikuwa akifanya kila ajisikiacho kutoa mipasho kwa wanao muita ‘Gold digger’. Katika harakati za kupost picha ndipo alipopost picha iliyomsababisha Diamond Platnumz aaze kusema ya juu ya nyumba yao ya Afrika Kusini. Moja kwa moja Diamond Platnumz alitupia comment kwenye moja ya picha ya Zari nakuandika “@zarithebosslady Can’t wait for the Launching of our new House in South Africa… I thing we gat to call it Tiffah’s Pallace or Tiffah’s Castle or The Embassy!!! ” Naye Zari akarudi ku comment kwakuandika “”@diamondplatnumz can’t wait my love for the new mansion our cast. The Chibus palace “

Simba yajigamba kuwashikisha adabu

Nyota wa Simba wakijifua kwenye mazoezi yao yanayoendelea mjini Morogoro, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.Source www.mwanaspoti.co

Genk yasonga Europa League

Usiku wa Julai 21 Genk ilikuwa uwanja wa ugenini kuikabili timu ya Buducnost kwenye michuano ya kuwania kupangwa hatua ya makundi ya michuano ya Europa League. Katika mchezo huo uliomalizika kwa kwa Genk kufungwa bao 2-0, ilibidi umauliwe kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 30 za nyongeza kumalizika kwa matokeo ya 2-0 yaliyosabaisha matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2. Ikumbukwe mchezo wa awali (Julai 14) takriban juma moja lililopita Genk ilipata ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani huku Samatta akifunga bao la pili. Samatta akicheza kwa dakika zote 120, alifunga moja ya penati ambazo ziliisaidia timu yake kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Mikwaju ya penati kwa upande wa Genk ilifungwa na Dries Wouters, Mbwana Samatta, Bryan Heynen na Thomas Buffel   na kuvusha Genk kwenda raundi ya pili kwa jumla ya penati 4-2. Genk itapambana na klabu ya Cork City kutoka Jamhuri ya Ireland katika raundi ya pili ya kutafuta tiketi ya kucheza Eu

KOVACIC ANUKIA TENA LIGI KUU YA ITALIA

 KUFUATIA ugumu wa namba katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid, huenda Mateo Kovacic akarudisha majeshi katika Ligi Kuu ya Italia, huku AC Milan ikiripotiwa kumtaka kiungo huyo kwa mkopo. Kovacic, 22, alitua Madrid akitokea Inter msimu uliopita kwa dau la pauni mil 31 na mabingwa hao wa Ulaya wanajipanga kumpiga bei mchezaji huyo kwa gharama ya pauni mil 36.

For TP Mazembe, the richest club in Africa, the future looks bright

For TP Mazembe, the richest club in Africa, the future looks bright Jamie Rainbow February 16, 2013 0shares TAGS: Entrance to T.P. Mazembe's entrance to their old administration centre September 3, 2012. Lubumbashi, Katanga Province, the Democratic Republic of Congo Their body language is not the earnest one of African charities, all big pleading eyes aimed at provoking a donation. Here in these young African schoolboys is defiance, pride, ambition. The first day of senior school for the latest intake at TP Mazembe’s academy is a chance, their chance. More than 8,000 children from across the DRC and neighbouring countries were scouted, given a chance to impress and take one of just a dozen places in an academy that has the potential to change their lives. “We have some boys here who are 12 or 13, that are very good but have never been to school for a single day, so we are paying their school fees,” says Régis Laguesse, director of the academy. The parents all h

ARGENTINA WAANDAMANA KWENYEMVUA KUSHINIKIZA MESSI KUREJEA KIKOSINI

KWA tafsiri ya haraka haraka, unaweza kusema kuwa wanasema asiwatanie, baada ya mamia wa raia wa Argentina juzi kuingia mtaani wakati mvua kubwa ikinyesha wakishinikiza nahodha wa timu ya taifa, Lionel Messi kurejea katika kikosi chao, baada ya kutangaza kustaafu kwa kufungwa katika mechi ya fainali ya Kombe la Copa America. Messi ambaye ni mchezaji bora wa dunia mara tano, amrewahi kucheza fainali tatu za Kombe la Copa America, ambazo ni za mwaka 2007, 2015 na 2016 pia na za Kombe la Dunia za mwaka 2014 na kupoteza zote. Wakati wa mechi ya fainali dhidi ya mahasimu wao Chile alikosa penati ya kwanza wakati wa hatua hiyo ikiwa ni baada ya miamba hao kushindwa kufungana. “Nadhani ndivyo ilivyo. Kibarua changu katika timu ya taifa kimemalizika,” staa huyo alimwambia mwandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika mechi. Hata hivyo, uamuzi huo haukuwaingia akilini watu mashuhuri nchini argentina, akiwemo rais wao Mauricio Macri na Diego Maradona, juzi jioni kujitokeza kwenye mzunguuk

MAKONDA AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Sophia Mjema (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Mhe.Sophia Mjema (kulia) akionesha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Hashim Mgandilwa (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Felix Lyaniva (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa

fainali ya Euro 2016 Ujerumani yasubiria mbabe leo

  Timu ya taifa ya Ujerumani imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Uero inayoendelea huko nchini Ufaransa baada ya kuifunga timu ya Italia. Ujerumani ambao ndiyo mabingwa wa kombe la dunia walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya taifa ya Italia kwa jumla ya penalti 6-5. Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimeshafungana goli 1-1 huku Ujerumani wakiwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 65 lililofungwa na Mesut Ozil, lakini dakika ya 78 Leonardo Bonucci aliisawazishia timu yake ya Italia bao hilo kwa njia ya penalti ndipo zikaongezwa dakika 30 hata hivyo hazikuweza kufungana tena. Mchezo huo ulionekana kuwa na penalti nyingi zikiwa ni jumla ya penalti 18, Ujerumani walikosa jumla ya penalti tatu nao Italia wakikosa penalti nne. Wachezaji wa Ujerumani waliokosa penalti ni pamoja na Thomas Muller, Mesut Ozil na Bastian Schweinsteiger huku kwa upande wa Italia wachezaji waliokosa penalti n

Simba imetangaza wakali wa 2016-17

Simba imekamilisha usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao (2016-17) ambao kwa asilimia kubwa imeufanya kimyakimya hususan ule wa wachezaji wa nje ya nch. majina yote ya wachezaji watakaohudumu kwenye msimu ujao kuanzia magolikipa hadi washambuliaji. Hiki hapa ni kikosi kamili cha ‘Wekundu wa Msimbazi;’ Goalkeepers: Foreign: Vincent De Paul Angban Peter Manyika Denis Deonis Right Back: Hamadi Juma: Coastal Union Salum Kimenya: Prisons Left Back: Mohamed Hussein Abdi Banda Centerback: Novaty Lufunga Foreign: Juuko Murushid Emmanuel Simwanza: Mwadui FC Foreign: Janvier Besala Bokungu Midfielders: Jonas Mkude Awadh Juma Foreign: Justice Majabvi Saidi Ndemla Mwinyi Kazimoto Mzamiru Yassin: Mtibwa Sugar Mohamed Ibrahim: Mtibwa Sugar Foreign: Mussa Ndusha Wingers: Peter Mwalyanzi Jamal Mnyate – Mwadui FC Shiza Kichuya – Mtibwa Sugar Hassan Kabunda – MwaduiFC Strikers: Ibrahim Hajibu Daniel Lyanga Haji Ugando Mbarak

Vijue vitu Vitatu alivyo vipiga vita RC Paul Makonda

Ni July 2, 2016 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku vitu vitatu kutoonekana katika mkoa wa Dar es Salaam. Akizungumza kwenye kongamano la Dini lililofanyika katika uwanja wa Taifa alisema..’ Kwanza kwa watumiaji wa biashara ya Sheesha katika maeneo ya Bar, Clubs na sehemu zingine kuanzia leo ni marufuku katika maeneo hayo’ ‘ Pili ni marufuku kwa wavutaji wa Sigara kwenye sehemu za wazi kwani wataalamu wanasema ule moshi unamuathiri yule asiyetumia hiyo Sigara kuliko yule anayetumia Sigara’ – Paul Makonda ‘ Tatu ni marufuku kwa ushoga kwenye mkoa wangu wa Dar es Salaam na mashoga wote walio kwenye instagram na Facebook watakamatwa na wale wote wanao wa follow mashoga kwenye mitandao ya kijamii basi watakuwa na hatia ile kama ya mashoga ‘

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) KUFUNGUA OFISI KIGALI,RWANDA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Joseph Pombe Magufuli. Na Daudi Manongi, MAELEZO. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Joseph Pombe Magufuli  amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) watafungua ofisi nchini Rwanda ili kuraisisha  uhakiki wa bidhaa  kwa  wafanyabiashara  wa  Rwanda wanaoingia nchini. Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame anafanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania ikiwemo ufunguzi wa Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam. Aidha amesema kuwa Serikali imetoa eneo la bandari kavu (ICD) kwa ajili ya kuhifadhia Bidhaa kutoka nchi ya Rwanda ili kupunguza urasimu ambao umekuwa kikwazo kwa maendeleo ya biashara hapa nchini na kwa namna hiyo biashara itakua kwani tunategemea uchumi utapanda kutoka asilimia 7 ya sasa mpaka asilimia 7.2. Pia amesema kuwa Serikali imepunguza vituo vya ukaguzi barabarani kutoka Tanzania kwenda Rwanda ku