Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Sophia
Mjema (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee
Jijini Dar es Salaam.
Mhe.Sophia
Mjema (kulia) akionesha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyokabidhiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) mara baada ya kuapishwa
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Hashim
Mgandilwa (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni leo katika Ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Felix
Lyaniva (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke leo katika Ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na
Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam (mbele) pamoja na Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam (nyuma)mara baada ya
kuisha kwa zoezi la kuapishwa lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa
Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Ally Hapi
(kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni leo katika Ukumbi wa Karimjee
Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewataka Wakuu wapya wa Wilaya
kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi waliopo katika Wilaya zao ili
kudumisha amani.
Makonda
alisema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakuu wa
Wilaya juu ya kuwalinda wananchi na mali zao na kuhakikisha usalama
unakuwepo katika Wilaya wanazozisimamia.
Alieleza
kuwa kwa kuwa wao ndio wanaomuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Wilaya zao, wanatakiwa
kuhakikisha wametekeleza ahadi zilizotolewa na Mhe. Rais wakati wa
kampeni.
“Ningependa
wakuu wangu wa Wilaya mchukiwe kwa kusimamia Haki na Sheria kuliko
kukumbatia uovu kwa kuhitaji furaha ya muda mfupi, hakikisheni Sheria na
Kanuni zilizopo kwenye Katiba ndio ziwe muongozo wenu”, alisema
Makonda.
Mkuu huyo
wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwataka Wakuu wa Wilaya zake kuwasimamia
Wakurugenzi wao ili kuhakikisha wanatumia bajeti waliyopewa katika
kutatua changamoto zilizopo katika Wilaya zao.
Aidha,
Makonda amewasisitiza kuhakikisha kuwa kuanzia Julai 11 mwaka huu maeneo
yote yanayofanya biashara ya shisha kufungwa na kuweka maeneo maalumu
kwa ajili ya kuvutia sigara.
Wakuu wa
Wilaya wapya wamepewa wiki mbili za kutengeneza mpango kazi kwa kusoma
ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hotuba ya Mhe.Rais John Magufuli
aliyoisoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania na mazingira ya kazi katika maeneo yao.
Comments