KUFUATIA ugumu wa namba katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid, huenda Mateo Kovacic akarudisha majeshi katika Ligi Kuu ya Italia, huku AC Milan ikiripotiwa kumtaka kiungo huyo kwa mkopo.
Kovacic, 22, alitua Madrid akitokea Inter msimu uliopita kwa dau la pauni mil 31 na mabingwa hao wa Ulaya wanajipanga kumpiga bei mchezaji huyo kwa gharama ya pauni mil 36.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Comments