KWA tafsiri ya haraka haraka, unaweza kusema kuwa wanasema asiwatanie, baada ya mamia wa raia wa Argentina juzi kuingia mtaani wakati mvua kubwa ikinyesha wakishinikiza nahodha wa timu ya taifa, Lionel Messi kurejea katika kikosi chao, baada ya kutangaza kustaafu kwa kufungwa katika mechi ya fainali ya Kombe la Copa America. Messi ambaye ni mchezaji bora wa dunia mara tano, amrewahi kucheza fainali tatu za Kombe la Copa America, ambazo ni za mwaka 2007, 2015 na 2016 pia na za Kombe la Dunia za mwaka 2014 na kupoteza zote. Wakati wa mechi ya fainali dhidi ya mahasimu wao Chile alikosa penati ya kwanza wakati wa hatua hiyo ikiwa ni baada ya miamba hao kushindwa kufungana. “Nadhani ndivyo ilivyo. Kibarua changu katika timu ya taifa kimemalizika,” staa huyo alimwambia mwandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika mechi. Hata hivyo, uamuzi huo haukuwaingia akilini watu mashuhuri nchini argentina, akiwemo rais wao Mauricio Macri na Diego Maradona, juzi jioni kujitokeza kwenye mzunguuko wa Obelisco, ambao ni mmoja wa viwanja vilivyo katikati ya mji wa Buenos Aires ambako kiutamaduni ndipo mashabiki huwa wanakusanyika kusheherekea ushindi katika michezo, ili kumshinikiza staa huyo abadili maamuzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Comments