Timu ya taifa ya Ujerumani imefanikiwa kutinga hatua ya nusu
fainali ya michuano ya Uero inayoendelea huko nchini Ufaransa baada ya
kuifunga timu ya Italia.
Ujerumani ambao ndiyo mabingwa wa kombe la dunia walifanikiwa kutinga
hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya taifa ya Italia kwa jumla ya
penalti 6-5.
Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimeshafungana goli
1-1 huku Ujerumani wakiwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 65
lililofungwa na Mesut Ozil, lakini dakika ya 78 Leonardo Bonucci
aliisawazishia timu yake ya Italia bao hilo kwa njia ya penalti ndipo
zikaongezwa dakika 30 hata hivyo hazikuweza kufungana tena.
Mchezo huo ulionekana kuwa na penalti nyingi zikiwa ni jumla ya
penalti 18, Ujerumani walikosa jumla ya penalti tatu nao Italia wakikosa
penalti nne.
Wachezaji wa Ujerumani waliokosa penalti ni pamoja na Thomas Muller,
Mesut Ozil na Bastian Schweinsteiger huku kwa upande wa Italia wachezaji
waliokosa penalti ni Matteo Darmian, Simone Zaza, Leonardo Bonucci n
a Graziano Pelle.
a Graziano Pelle.
Sasa Ujerumani atakutana na mshindi wa mechi ya leo kati ya wenyeji Ufaransa na timu ya taifa ya Iceland.
Comments