Kampuni ya internet ya Marekani, Yahoo imenunuliwa na kampuni
ya mawasiliano ya Verizon Communications kwa dola bilioni 5, fedha
taslimu.
Yahoo itaunganishwa na AOL, kampuni nyingine ya internet iliyopoteza
umaarufu ambayo nayo ilinunuliwa mwaka jana na kampuni hiyo. Hata hivyo
dili hilo halijumuishi hisa za thamani ilizonazo kwenye kampuni ya
China, Alibaba.
CEO wa Yahoo, Marissa Mayer
Fedha hizo ni ndogo zaidi kuliko dola bilioni 44 ambazo kampuni ya
Microsoft ilitaka kuinunua Yahoo mwaka 2008. Yahoo iligoma kununuliwa
kwa kiasi hicho cha fedha. Enzi za umaarufu wake, Yahoo ilikuwa na
thamani ya dola bilioni 125.
CEO wa saba na wa mwisho wa Yahoo, Marissa Mayer, anadaiwa kuwa
ataondoka baada ya dili hilo huku akilipwa kiinua mgongo cha dola
milioni 50.
Comments