Usiku wa Julai 21 Genk ilikuwa uwanja wa ugenini kuikabili timu
ya Buducnost kwenye michuano ya kuwania kupangwa hatua ya makundi ya
michuano ya Europa League.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa kwa Genk kufungwa bao 2-0, ilibidi
umauliwe kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 30 za nyongeza
kumalizika kwa matokeo ya 2-0 yaliyosabaisha matokeo ya jumla kuwa sare
ya 2-2.
Ikumbukwe mchezo wa awali (Julai 14) takriban juma moja lililopita
Genk ilipata ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani huku
Samatta akifunga bao la pili.
Samatta akicheza kwa dakika zote 120, alifunga moja ya penati ambazo
ziliisaidia timu yake kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Mikwaju ya
penati kwa upande wa Genk ilifungwa na Dries Wouters, Mbwana
Samatta, Bryan Heynen na Thomas Buffel na kuvusha Genk kwenda raundi ya pili kwa jumla ya penati 4-2.
Genk itapambana na klabu ya Cork City kutoka Jamhuri ya Ireland
katika raundi ya pili ya kutafuta tiketi ya kucheza Europa League hatua
ya makundi.
Comments