Wanasiasa, Zitto Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad kwa pamoja
wameitwa jijini Philadelphia, Marekani kwaajili ya kuhudhuria mkutano
mkuu wa chama cha Democratic.
Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Wanasiasa hao wameitwa kuhudhuria mkutano mkuu wa cha hicho
utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa Marekani kupitia
chama hicho.
Marekani inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Novemba 8 mwaka huu ambapo
Clinton atathibitishwa kwenye mkutano huo kuchuana na Donald Trump wa
chama cha Republican.
Akizungumza na gazeti la Mwanahalisi, Ofisa Habari wa ACT- Wazalendo,
Abdallah Khamis, amesema, “wakati Zitto akiwa kwenye mkutano huo,
atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa
duniani.”
“Kufanya kikao cha maandalizi juu ya ufunguzi wa tawi la wanachama wa
ACT Diaspora la nchini Marekani pamoja na kuwa na mazungumzo maalum na
Maalim Seif juu ya hali ya kisiasa ya Zanzibar na taifa kwa ujumla,”
aliongeza.
Viongozi hao ndio wanasiasa pekee nchini waliopata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.Source Bongo5
Comments