Kuelekea
mkutano mkuu wa Simba unaotaraji kufanyika Jumapili ya Julai, 31,
shabiki na mkeleketwa wa Simba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa
Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji
amezungumza mipango yake aliyopanga kuifanyia Simba kama akipata nafasi
ya kununua hisa asilimia 51 za klabu hiyo.
MO
amesema kuwa mipango yake ni kuwekeza Bilioni 20 na amepanga bajeti ya
klabu hiyo kwa mwaka iwe Bilioni 5.5, kiasi ambacho anaamini kuwa
kitaweza kubadili mwelekeo wa Simba kutoka ilivyo sasa na kurudisha zama
zake za kutwaa mataji ya ndani na kufika hatua nzuri kimataifa.
MO
alisema amefikia uamuzi wa kutaka kununua hisa katika klabu ya Simba
kutokana na mapenzi aliyonayo katika klabu hiyo na hana nia yoyote ya
kiabiashara na klabu hiyo kwani tayari ana biashara anazofanya ambazo
zinamuingizia pesa nyingi hivyo jambo hilo ni kuona timu aliyo na
mapenzi nayo ikifanikiwa.
“Nipo
tayari kuwekeza Bilioni 20 kama watanipa nafasi lakini tukubaliane kuwa
hakuna mtu atagusa pesa hizo pesa, tutauza bondi na kwa kila mwaka
tutaingiza Bilioni 3.5 na tutatengeneza mapato ya Bilioni 2 kila mwaka
ukijumlisha ni Bilioni 5.5 ambayo itakuwa ni bajeti ya mwaka,
“Inaniuma
sana kuona klabu imekuja juzi tu leo inatuzidi mafanikio lakini kama
Yanga na Azam bajeti zao kwa mwaka ni Bilioni 2.5 hadi Bilioni 3, sisi
tukiwa na bajeti ya Bilioni 5.5 tutakuwa tumewazidi na tutaleta
wachezaji wazuri na kocha mzuri,” alisema na kuongeza.
“Dhamira
yangu sio kupata Simba kibiashara, mimi Mungu kanijalia nina pesa nina
biashara ziadi ya 100, tumeajiri wafanyakazi wanafika 28,000 , jambo
ninalolitaka Simba ni kuwekeza, tubadili mfumo, tushinde mataji na sio
Tanzania pekee shabaha yangu ni kushinda mataji ya Afrika”
Aidha
MO alisema kuwa kama akipata nafasi atazungumza na viongozi wa Simba
ili kila mwanachama wa klabu wa muda mrefu apatiwe hisa bure kutokana na
kazi kubwa ambayo wameifanya katika klabu hiyo.
“Nitazungumza
na viongozi wa klabu tuone jinsi ambavyo tunaweza kuwapa bure wanachama
wa klabu ambao wamekuwa na timu kwa muda mrefu, wameshatoka jasho sana
na Simba hivyo tutawapa hisa za timu bure,” alisema MO.
Hata
hivyo MO aliongeza kuwa yupo tayari kwa lolote kama katika mkutano mkuu
wa Jumapili watamnyima nafasi ya kuwekeza katika klabu ya Simba na
kueleza kuwa anachoamini kwa sasa Simba haiitaji mdhamini bali Simba
inahitaji mwekezaji.
“Mimi
wakininyima kwa moyo mweupe kabisa sina tatizo na hili jambo hata
likifanikiwa halitakamilika kesho linaweza kuchukua muda sababu kuna
mambo ya kufanyiwa marekebisho na kusaini mikataba ila kama nikiona
mambo yanakwenda sawa kwa hicho kipindi nitaangalia jinsi gani
nitaisaidia Simba sababu nina mapenzi nayo,” aliongeza MO.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments