Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2018

Pierre-Emerick Aubameyang leo ametia saini mkataba wa muda mrefu kuichezea klabu ya Arsenal

Mshambuliaji wa klabu ya Borrussia Dortmund ya Ujerumani raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang leo ametia saini mkataba wa muda mrefu kuichezea klabu ya Arsenal. The Gunners waliwasilisha maombi mawili ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambayo yalikataliwa na Dortmund kabla ya kukubali dau la juu ya £46.5m walilomsajilia Alexandre Lacazette. Klabu ya Arsenal imeandika kwenye mtandao wao kwamba Aubameyang ni Mchezaji wao wa pili kumnunua katika kipindi cha kuhama wachezaji mwezi Januari.

Maida Waziri:akagua bidhaa za kinana mama wajasiriamali

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Contraters Limited na Rais wa Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania VOWET Maida Waziri,akikagua bidhaa za kinana mama wajasiriamali.  wakina mama walioshiriki kwenye Jukwaa la wanawake katika kata ya Keko jijini Dar es salaam wakiwa wameshika mabango ya maandamano. Mgeni rasmi  Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Contraters Limited na Rais wa Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania VOWET Maida Waziri akiendelea kukagua bidhaa za wajasiriamali Ilikuendelea kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda Wanawake nchini wametakiwa kujishughulisha katika ufanyaji wa kazi mbalimbali ili kuweza kujipatia kipato na kuleta mapinduzi ya uchumi kwa wanawake. Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Contraters Limited na Rais wa Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania VOWET Maida Waziri,ameyasema hayo leo alipokuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la wanawake wa keko ambalo limefanyika kwenye kata ya Keko jiji Dar es salaam. Maida amesema ni vyema kinamama wakajiwekea maz

DR. Kigwangala asikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili wachongaji wa vinyago

Waziri wa maliasili na utalii hapa nchini DR.Hamis Kigwangala(picha na mtandao)   Dar es salaam Waziri wa maliasili na utalii hapa nchini DR.Hamis Kigwangala leo amezungumza na   wafanyabiashara na wachongaji wa vinyago katika eneo la Mwenge jijini Dar es salaam, katika ziara yake hii leo,   ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye mchango mkubwa kwenye utalii na kuliingizia taifa kipato. Baada ya kuwasili katika  eneo hilo na kutembelea baadhi ya mabanda mbalimbali ya sanaa hiyo,  Dk.Kigwangala amesikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili wachongaji wa vinyago. Dk.Kigwangala amewataka wafanyabiashara hao kumaliza changamoto zao, ili serikali iweze kurahisisha mipango juu ya wachongaji na wafanyabiasahara wa eneo hilo. Dk.Kigwangala aliendelea na ziara yake ambapo pia hii leo amewatembelea wasanii wa sanaa ya uchoraji manispaa ya kinondoni katika eneo la Morogoro store maarufu tingatinga,  na kusema kuwa seriakali kupitia utalii inataka kila mwananchi kuweza kufa

HAKUNA RUFAA YA UCHAGUZI WA LONGIDO ILIYOPO MAHAKAMANI

Mahakama ya Rufaa imesema hakuna rufaa ya uchaguzi wa Jimbo la Longido iliyopo mahakamani hapo. Mahakama imetoa kauli hiyo wakati Chadema ikiilalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu kufanyika uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo kwa madai kwamba kuna kesi mahakamani hapo. Uchaguzi huo mdogo ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Longido kwa tiketi ya Chadema, Onesmo ole Nangole ushindi wake kutenguliwa na Mahakama Kuu. Mara kadhaa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Ole Nangole wamekaririwa na vyombo vya habari wakidai kwamba kuna rufaa katika Mahakama ya Rufani.  Viongozi hao wamekuwa wakiilalamikia NEC kuwa iliendesha uchaguzi mdogo katika jimbo hilo wakati rufaa ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomvua ubunge Ole Nangole ikiwa haijatolewa uamuzi. Mahakama ya Rufaa imesema uchaguzi mdogo uliofanyika Longido ulikuwa halali kwa kuwa hakuna rufaa yoyote iliyoko mahakamani hapo. Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Elizabeth Mkwizu a

Moto wazuka katika hospitali ya mji mdogo wa Miryang

Moto wazuka katika hospitali ya mji mdogo wa Miryang kusini-mashariki mwa nchi umesababisha maafa mengi. Moto mkubwa uliozuka leo Ijumaa katika hospitali moja nchini Korea Kusini, umeua watu wasiopungua 41 kwa mujibu wa shirika la habari la Yonhap, maafa mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja. Watu zaidi ya 80 wamejeruhiwa pia katika janga hili linalotokea wiki moja kabla ya kuwasli nchini humo maelfu ya wanariadha na wageni kwa mashindano ya Olimpiki ya Majira ya baridi. Katika video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya wagonjwa waliokolewa na helikopta kwa kutumia kamba juu ya hospitali ya Miryang kusini-mashariki mwa Korea Kusini. Na wengine wamekua wakiokolewa kwa kupitishwa kwenye madirisha mbalimbali. Moto umezuka katika hospitali ya Miryang, Kusini-Mashariki mwa Korea Kusini: wagonjwa waokolewa.Kim Dong-min/Yonhap via REUTERS Jengo hilo la ghorofa sita lina sehemu wanakohudumia wazee pamoja na sehemu ya hospitali. Idad

Mshindi wa gali katika shindano la Misuli Majura aanza kujipanga kutimkia Nigeria

MSHINDI wa shindano la kutunisha misuli Erick Majura amsema mara baada ya kutwaa ushindi katika ukumbi wa Mayfair jijini Dar es Salaam Desemba mwaka jana bado anaendelea kujiweka fiti kuelekea shindano jingine litakalo fanyika nchini Nigeria. Hali hiyo inakuja baada ya mwishoni mwa mwaka jana ambapo shirikisho  la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF) kwa kushirikiana na Kampuni waandaaji wa shindano hilo Pilipili intertainment kuandaa vema shindano hilo. Majura alisema baada ya kuwa mshindi na kuweza kutwaa gali na kitita cha sh.Milion 10,000 kwa kuwagalagaza vibaya wenzake walioshiriki ,  taswira yake kwa sasa inawazia kuendelea mbele zaidi ambapo anajiandaa kwenda kushiriki shindano kubwa la Afrika katika mchezo huo wa misuli. "Najua tutakwenda kuchuana na wenzangu wenye sifa kama mimi , tayari naendelea kujipanga kwa kufanya mazoezi vema katika mazoezi yangu ya kila siku kwa mwenyezi Mungu ni mkubwa na shukuru sana kwa kuwa mshindi kwa mwaka jana

Serikali yasitisha Shughuli za Kampuni Tatu

Serikali yasitisha Shughuli za Kampuni Tatu (3) za Wakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini kutokana na kukiuka matakwa ya sheria ya huduma za ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni zake. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali kuhusu utaratibu unaotumiwa na baadhi ya wakala binafsi wa huduma za ajira nchini. Kampuni zilizofutiwa usajili baada ya kukiuka sheria ni pamoja na Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre Agency na Competitive Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala  binafsi wa ajira  nchini. Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa uchunguzi umebaini ukiukwaji wa taratibu za usajili ambapo baadhi ya mawakala wamekuwa wakitumia nyaraka zilizopatikana kwa njia isivyo halali katika kujipatia leseni za uwakala hali iliyowa

Magazeti ya leo

Staa huyu atangaza kolabo na Quavo

Iggy Azalea amekuwa na wakati mgumu katika kuachia albamu yake ya Digital Distortion, albamu hiyo ilitakiwa kutolewa tarehe 30 Juni mwaka jana lakini ilipigwa chini na Def Jam Records. Msanii huyo alidai kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Def Jam Steve Bartels amekataa kuachia ngoma zake na tukio hilo lilitokea baada ya ngoma yake ‘Switch’ aliyomshirikisha mbrazil aitwaye Anitta kushindwa kufanya vizuri. Iggy sasa ameamua kuanza upya katika mwaka huu kwa kutangaza kuachia ngoma iitwayo ‘Switch’.Raia huyo wa Australia ametangaza leo kwamba ngoma hiyo atamshirikisha msanii Quavo kutoka kwenye kikundi cha Migos. Msanii huyo ametangaza kuwa tarehe 1 Februari mwaka huu ndio siku atakayo iachia ngoma hiyo, Iggy pia amethibitisha kufanya kolabo hiyo na Quavo kwa kumjibu shabiki wake katika mtandao wa Twitter. Iggy ameonyesha picha ya nyimbo hiyo ambayo ataiachia rasmi Februari 2 mwaka huu. View image on Twitter IGGY AZALEA ✔ @IGGYAZALEA # SAVIOR FEB 2nd... The c

Upelelezi wa kesi Jamali Emil Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Swelestine wakamilika

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamekwisha kamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili waliyokuwa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Viongozi hao wanaokabiliwa na mashataka ni pamoja na aliyekuwa rais wa TFF, Jamali Emil Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Swelestine, na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga. Washitakiwa hao walipandishwa kizimbani kwamara ya kwanza Juni 29 mwaka 2017 wakikabiliwa namashtaka 28 ya kuhujumu huchumi ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. Kesi hiyo imeghairishwa hadi Februari 8 mwaka 2018.

NHC: Yakabidhi nyumba za makazi

Meneja wa Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Itandula Gambalagi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa na Kamishna wa Fedha, Ndugu Peter Chogero kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wakikabidhiana hati ya makabidhiano ya nyumba baada ya kukabidhi nyumba 63 kwa Jeshi la Uhamiaji. Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji. Picha ya pamoja ya uongozi wa Shirika la Nyumba na Uhamiaji baada ya makabidhiano ya nyumba 63 za makazi katika mradi wa Iyumbu Satellite Center. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi nyumba za makazi zilizojengwa kwenye mradi wa kitovu cha mji wa kisasa wa nyumba za gharama nafuu wa Iyumbu Satellite Centre kwa Idara ya Uhamiaji.

Mhe Freeman Aikael Mbowe amefika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi

Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anakabiliwa na kesi kutoa maneno ya uchochezi.

Novak Djokovic atinga nusu fainali kwa kishindo

Mcheza tenesi kutoka Korea Kusini Chung Hyeon amefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Australian Open 2018. Chung ametinga kwenye hatua hiyo baada ya kumtupa nje ya mashindano hayo Tennys Sandgren kwa seti 6-4 7-6 (7-5) 6-3. Awali mchezaji huyu anayeshika nafasi ya 58 katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani hakupewa nafasi hata kidogo kufikia katika hatua hiyo huku akimtupa nje ya michuano hiyo kigogo Novak Djokovic Jumatatu hii kwa seti 7-6, 7-5, 7-6. Chung Hyeon amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Korea Kusini kufika katika hatua kama hiyo ya michuano hiyo.

Uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita

Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uteketezaji wa zana haramu za uvuvi kwenye Kijiji cha Nkome Wilayani Geita . Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akielezea mikakati ya wilaya ya kuhakikisha wanapamba zaidi na vitendo ambavyo vimeendelea kufanywa na wavuvi ambao awana mapenzi mema na samaki waliomo kwenye ziwa viktoria wakati wa zoezi la uteketezaji wa zana haramu.  Wananchi wa Kata ya Nkome wakiwa kwenye mkutano ambao ulikuwa na lengo la kuelezea hali ya uvuvi haramu ilivyo kwenye kata ya Nkome na namna ambavyo oparesheni imeweza kufanyika kwenye maeneo hayo.  Kiongozi wa kikosi maalumu kinachoendesha oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu ziwa victoria Gabriel Mageni akielezea namna ambavyo wameweza kuendesha zoezi hilo ndani ya siku kumi na mbili.  Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisita kwa wale ambao ni watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu . Na Joel Maduka,Geita

Wahimizwa kuchangamkia fursa Visiwa vya Comoro

Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe, Sylvester Mabumba (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji wa Comoro, Bw. Said Mohamed Omar (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group pamoja na wajumbe waliofuatana nao katika ziara maalum ya kufungua na kuzitangaza fursa zilizopo Tanzania na Comoro. WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA COMORO Balozi wa Tanzania katika Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba alipokea ujumbe wa Clouds Media Group uliowasili visiwani humo  tarehe tarehe 20 Januari 2017 kwa ziara maalumu ya siku tatu ikiwa na lengo la kushirikiana na Ubalozi kuzitangaza fursa mbalimbali zinazopatikana Visiwani humo kwa Watanzania.    Ujumbe huo wa Clouds Media Group ukiongozwa na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Bw. Ruge Mutahaba uliwasili Comoro kufuatia mualiko wa Ubalozi wa Tanzania hapa Comoro ambapo lengo la