Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wamekwisha kamilisha upelelezi wa kesi inayowakabili waliyokuwa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Viongozi hao wanaokabiliwa na mashataka ni pamoja na aliyekuwa rais wa TFF, Jamali Emil Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Swelestine, na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga.
Washitakiwa hao walipandishwa kizimbani kwamara ya kwanza Juni 29 mwaka 2017 wakikabiliwa namashtaka 28 ya kuhujumu huchumi ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. Kesi hiyo imeghairishwa hadi Februari 8 mwaka 2018.
Comments