Kampuni ya Reli Tanzania imesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyeesha katika maeneo mbalimbali nchini zimesababisha uharibifu wa miundombinu ya Reli ikiwemo reli ya stesheni za Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma.
Uongozi wa kampuni hiyo umesema kutokana na mafuriko ya mvua zilizonyeesha kwenye maeneo hayo imepelekea huduma za reli kutoka jijini Dar es salaam kusitishwa kufanya shughuli za usafirishaji wa abiria.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa TRL Dar es Salaam juzi ,Kaimu Naibu Mkurugenzi wa uendeshaji wa reli Tanzania,FOCUS MAKOYE SAHANI amesema wametathmini hali hiyo na kuhamishia huduma ya usafiri kutokea Dodoma kuanzia siku ya jumanne Januari 16,2018
Kwa upande wake Meneja ulinzi na Usalama wa Reli Gukwi Michael amesema kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi ya watu kulima karibu na reli jambo ambalo linasababisha maji kuwa mengi katika miundomibinu ya reli.
TRL bado inaendeleza juhudi za kusimamia kazi ya ukarabati wa eneo lililoharibika kati ya Kilosa na Gulwe ili huduma za usafiri wa reli ziendelee kama kawaida.
Comments