Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoishi kwenye mpaka kati ya Buguruni Mivinjeni, Sharifu Shamba pamoja na Mtoni kwa Azizi Ali kuwa watunzaji wazuri wa mitaro ya maji kwani ni mali yao wenyewe na si ya serikali.
Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kuta za bahari na mitaro ya maji jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi hao kuwa mabadiliko ya tabia nchi yameathiri shughuli za kiuchumi , kijamii na kimazingira hivyo kila mmoja anapaswa kujishughulisha katika suala la kusafisha na kuhifadhi mazingira .
“Ubaya wa mazingira ukiyaharibu yanakuadhibu” alisisitiza na kuongeza kuwa nchi inapozungumzia uchumi wa viwanda ni mazingira “tukiharibu mazingira hamna uchumi wa viwanda” hata viwanda vitakavyojengwa vinahitaji kutunza mazingira, visafishe maji yake kabla ya kutiririsha.
Makamu wa Rais alitoa rai kwa yeyote atakayebainika kuharibu miundo mbinu wanachukuliwa hatua za haraka.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments