IGP Simon Sirro amtia saini ya makubaliano na mkuu wa jeshi la polisi la Msumbiji IGP Bernadino Rafael kwa lengo la kuhirikiana
Mkuu wa jeshi la polisi nchi IGP Simon Sirro jana alitia saini ya makubaliano na mkuu wa jeshi la polisi la Msumbiji IGP Bernadino Rafael kwa lengo la kuhirikiana katika kubaini wahalifu ,kuzuia na kupambana na uharifu.
Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam ambapo IGP Sirro amesema kuwa wamekubaliana kuzui na kupambana na wahalifu wanaofanya uharifu Tanzania na wanaofanya uharifu Msumbiji hasa uhalifu wa kigaidi,madawa ya kulevya na makosa mengine.
IGP Sirro amebainisha kuwa wahalifu mbalimbali nchini ikiwamo wa kibiti baada ya kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na jeshi la polisi wamekimbilia msumbiji na inadaiwa kuwa watu wanne tayari wamefariki dunia.
kwa upande wake Mkuu wa jeshi la polisi nchini msumbiji IGP Bernadino Rafael amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuishi kwa amani na uhuru na kubainisha kuwa hakuna magaidi watakaopata nafasi katika nchi hizo mbili.
Hata ivyo wananchi wa nchi hizo mbili wametakiwa kuonyesha umoja na mshikamano kwa jeshi la polisi ikiwemo kutoa taarifa za wahalifu pindi watakapo wabaini katika maeneo yao.
Comments