Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dr Ali Mohamed Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
Watanzania wanaadhimisha miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar, mapinduzi yaliyoshuhudia kuangushwa kwa utawala wa Sultan siku kama ya leo mwaka 1964.
Akiongoza maadhimisho hayo, rais wa Zanzibar Mohammed Shein amesema tangu kuondolewa kwa Sultan, Zanzibar imepiga hatua katika kupambana na umasikini, siasa na masuala ya usalama.
Zaidi ya wanamapinduzi 800 walishiriki kwenye mapinduzi hayo yaliyoifanya Zanzibar kuwa huru na baadaye kujiunga na Tanganyika kuunda Tanzania.
Pamoja na mafanikio hayo, Wazanzibari bado wanashuhudia changamoto za kisiasa, hasa wakati wa uchaguzi wa urais kati ya chama tawala CCM na kile cha upinzani CUF.
Comments