KIBAO ‘Jiamini’ ambacho ni utunzi wake mrembo Amina Remmy ndio habari ya mjini kwa sasa Tunduru mkoabni Songea ambako Ivory Band imeweka kambi hadi Februari mwishoni.
Kibao hicho kilichoko katika miondoko ya Zouk Rhumba kinafanya idadi ya nyimbo za Ivory Band wakiwa kambini kufikia saba hadi sasa ambapo ni albamu kamili ya bendi hiyo iliyo chini ya mwimbaji Salleh Kupaza.
Vibao vingine ni ‘No Stress’, ‘Nakupenda’, ‘Majibu ya Karaha’, ‘Baby Baby’ na ‘Ndo Basi Tena’.
Kwa mujibu wa Amina Remmy ambaye ni mkurugenzi mdogo wa Ivory Band, watakapovunja kambi na kurejea jijini Dar es Salaam watafikia moja kwa moja kurekodi na kufanya utambulisho wa nyimbo hizo na bendi yao kwa ujumla.
Comments