Luke
Shaw anaelekea kuwa mmoja kati ya mabeki bora kabisa wa Premier League
baada ya 'kufufua' kiwango chake Manchester United. Hayo ni maneno ya
Jose Mourinho.
Beki
huyo wa kushoto wa England ameanza katika mechi tano za mwisho za
Manchester United - hatua bora zaidi kwake tangu alipovunjika mguu
katika mechi dhidi ya PSV Eindhoven Septemba 2015.
Luke Show anatarajiwa pia kuanza katika mchezo wa Premier League Jumamosi hii dhidi ya Burnley licha Ashley Young kumaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu.
Mourinho hakumkubali Shaw msimu uliopita ambapo alimshutumu hadharani kwa kusema si mwajibikaji.
Hata
msimu huu ulipoanza bado Shaw hakuwa chaguo la kwanza wala la pili kwa
Mourinho huku kocha huyo akiwa anahusishwa na usajili wa beki wa kushoto
wa Tottenham Danny Rose kwa pauni milioni 27.
Wakati
dirisha la usajili la Januari lilipokaribia ndipo Mourinho alipompa
nafasi Shaw na yeye bila ajizi akadhidhirisha ubora wake uwanjani hadi
kumsuuza roho kocha huyo wa Manchester United.
Mourinho
alipoulizwa kuhusu beki huyo mwenye umri wa miaka 22, akasema:"Kwa muda
huu sioni mabeki wengi wazuri wanaomzidi Luke Shaw.
"Amekuwa
akicheza vizuri mno. Amecheza vizuri na kuimarika tangu nilipoanza
kumchezesha baada ya kukaa muda mrefu sana bila kuchezeshwa."
Comments