Zaidi ya robo tatu ya mashabiki wa Real Madrid wanataka Cristiano Ronaldo aondoke Real Madrid.
Kura za mtandaoni zilizopigwa na gazeti la Hispania AS, likafichua kuwa asilimia 67.5 ya watu 125,000 waliopiga kura hawataki Ronaldo abakie Bernabeu.
Hata hivyo kwa upande mwingine, kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane amesema haoni ni namna gani Real Madrid itakuwa bora bila Ronaldo.
Ronaldo hana furaha na namna Real Madrid wanavyoyeyusha kutekekeleza ahadi yao ya kumpa mkataba mpya wenye maboresho makubwa ya maslahi na sasa anahusishwa na safari ya kurejea Manchester United.
Nyota huyo wa Ureno ana mkataba Real Madrid hadi mwaka 2021 na Zidane amemtaka mshammbuliaji huyo arejeshe akili yake uwanjani.
Zidane alisema: "Tunajua kilichojadiliwa, lakini kile Cristiano anachofaa kufanya ni kufikiria kucheza kama kawaida. Yeye ni sehemu ya klabu hii, ndio sehemu inayomstahili. Anapendwa na klabu pamoja na mashabiki wake".
Comments