Wajumbe wa kamati ya mwezi wa maadhimisho ya urithi wa mtanzania Wakiongozwa na waziri wa maliasili na utalii Dr Hamis Kigwangala.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam
Ili kuendeleza na kukuza sekta ya utalii wa ndani na nje ya nchi wizara ya maliasili na utalii imeunda kamati ya mwezi wa maadhimisho ya urithi wa mtanzania yenye lengo ya kuboresha sekta hiyo.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wanakamati uliofanyika leo jijini Dar es salaam waziri wa maliasili na utalii Dr Hamis Kigwangala amesema kuwa urithi wa taifa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii Tanzania ambapo sekta ya utalii imechangia dola bilioni 2.1 na asilimia 25 ni fedha za kigeni.
Dk.Kigwangala amesema kuwa maadhimisho ya urithi wa mtanzania lengo lake kuwezesha jamii za watanzania kutimiza urithi wao ambao Tanzana imejaaliwa lakini pia kuzikumbusha jamii mila na tamaduni zao.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema katika mkoa wake kuna vivutio vingi na na kubainisha kuwa asilimia 80 ya mapato ya utalii nchini yanatoka mkoa wa Arusha
Kwa upande wake Kiongozi wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM ambaye pia ni Mwigizaji wa Filamu nchini Joketi Mwegelo amesema mchakato huo utasaidia kukuza na kuendeleza sekta ya Utalii nchini.
Ikumbukwe kuwa mkataa kwao mtumwa hivyo Watanzania ni vyema kuzilinda maliasili za taifa na kuzienzi tamaduni ili kuongeza pato la taifa na kukuza sekta ya utalii nchini.
Comments