Serikali Nigeria imeanza kusaka watu maarufu wanaokwepa kodi, na wiki hii wakusanya kodi wa Lagos Nigeria wameanza uchunguzi wa kodi zilizokwepwa na msanii maarufu Davido
Lagos State Internal Revenue Service (LIRS) wamefungua kesi dhidi ya msanii David Adeleke aka Davido na mchekeshaji AY ambao wanasema wamekuwa wakikwepa kulipa kodi kwa muda mrefu.
Davido ana dili kubwa na kampuni kama Sony Music Entertainment na ni balozi wa bidha kubwa Nigeria.
Kesi hii imefunguliwa baada ya Davido kusema ametengeneza Naira milioni Mia tano (500,000,000) katika matamasha yake ya mwezi December tu.
Watu wa Davido wanasema staa huyu analipa kodi katika mji wa Osun sababu ndipo anapotokea.
Comments