CHADEMA yapata pigo Muslim Hassanali na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ametangaza kujivua uanachama
Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Muslim Hassanali na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho leo Januari 9, 2018 ametangaza kujivua uanachama ndani ya CHADEMA na kujiunga na CCM.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amemtangaza kiongozi huyo leo katika Mkutano wa CCM ambao umefanyika Pugu jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa kitendo cha kuondoka kwa Muslim ni wazi kuwa ruzuku sasa zinaweza zisipatikane CHADEMA kwa kuwa ili zitoke lazima mtu huyo atie saini.
"Leo tumpokea Muslim Hassanali ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ni mjumbe wa bodi ya wadhamini na ni kati ya watia saini wawili wa CHADEMA ili ruzuku ipatikane ndani ya chama chao. Kuja kwake kwetu saizi ina maana tunajua mipango ya chama hicho na nguvu kubwa iliyokuwa inafanywa kuhujumu kazi kubwa mnayofanya nyinyi viongozi" alisema Polepole
Aidha Polepole amesema kuwa toka mwaka 2015 walipofanya mageuzi ya chama mpaka sasa wamefanikiwa kuongeza wanachama wapya wa CCM milioni mbili.
Comments