Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Contraters Limited na Rais wa Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania VOWET Maida Waziri,akikagua bidhaa za kinana mama wajasiriamali.
wakina mama walioshiriki kwenye Jukwaa la wanawake katika kata ya Keko jijini Dar es salaam wakiwa wameshika mabango ya maandamano.
wakina mama walioshiriki kwenye Jukwaa la wanawake katika kata ya Keko jijini Dar es salaam wakiwa wameshika mabango ya maandamano.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Contraters Limited na Rais wa Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania VOWET Maida Waziri akiendelea kukagua bidhaa za wajasiriamali
Ilikuendelea kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda Wanawake nchini wametakiwa kujishughulisha katika ufanyaji wa kazi mbalimbali ili kuweza kujipatia kipato na kuleta mapinduzi ya uchumi kwa wanawake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Contraters Limited na Rais wa Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania VOWET Maida Waziri,ameyasema hayo leo alipokuwa mgeni rasmi katika Jukwaa la wanawake wa keko ambalo limefanyika kwenye kata ya Keko jiji Dar es salaam.
Maida amesema ni vyema kinamama wakajiwekea mazoea ya kufanya shughuli mbalimbali za kijasiriamali ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano isemayo Tanzania ya viwanda inawezekana.
Kwa Upande wake Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Keko Agnes Soso amesema wamekuwa wakiwasaidia wanawake kwa kuwapatia mikopo ili iweze kuwasaidia katika shughuli zao wanazozifanya.
Oliver Joseph ni Mratibu wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Manispaa ya Temeke,amesema lengo la kuanzishwa majukwa ni kuwaunganisha wanawake pamoja ili waweze kuzungumzia changamoto zao nakuweza kupatiwa ufumbuzi.
Hata hivyo wanawake wamekumbushwa kushiriki katika kujifunza elimu ya ujasiriamali kwani ni ndio jambo litakalowawezesha kufanikiwa kukuza uelewa wa kibishara.
Comments